24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Miss Tanzania 2018 Queenelizabeti apata ubalozi JATU

Na Jeremia Ernest, Dar es Salaam

Kampuni ya Jenga Afya Tokomeza Umaskini ( JATU) PLC imemtangaza Miss Tanzania 2018, Queenelizabeth Makune kuwa balozi wake kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa ajili ya kuhamasisha kampeni mpya ya Uni talk inayolenga kuwafikia zaidi wanafunzi wa vyuo.

Akizungumza leo Dar es Salaam, Januari 14, Mkurugenzi wa JATU PLC, Peter Isare amesema wameingia mkataba wa mwaka mmoja na Queenelizabeth ili iwe rahisi kuwafiki wanachuo katika kampeni yao ya Uni talk.

“Queenelizabeth ni Miss Tanzania 2018 ni binti mwenyewe ushawishi katika jamii leo tumempa ubalozi katika kampuni yetu ya Jatu kupitia kampeni ya Uni talk, ambayo itahusisha vijana waliyopo katika Vyuo vyote nchini,” anasema Isare.

Kwa upande wake, Queenelizabeth, ameishukuru kampuni hiyo kwa kumpatia ubalozi na kuwataka vijana waliyopo vyuo na waliomaliza kujiongeza wajiunge na Jatu kwa ajili ya kuongeza wigo wa ajira katika sekta ya kilimo.

“Kuna vijana wengi ambao wamemaliza chuo wapo nyumbani hawana ajira, Jatu ipo kwa ajili ya kuongea ajira kwa upande wa kilimo, nitoe rai kwao na ambao bado wapo kwenye masomo kujiongeza ili waweze kufikia malengo yao katika ajira kuacha kuwa tegemezi,”amesema Queenelizabeth.

Ameongeza kuwa, mpaka sasa sekta ya kilimo imetoa ajira zaidi ya 50,000 hapa nchini, hivyo wakulima wanapaswa kufanya kilimo kinacho kwenda na wakati.

Kampuni ya Jenga Afya Tokomeza Umaskini ( JATU) PLC ni kampuni ya kitanzania, inayowaunganisha wakulima na kuwawezesha kulima kisasa na baada ya mavuno kampuni hununua mazao yote na baadaye kuandaa bidhaa ambazo huuzwa kwa wanachama wa JATU kwa mfumo wa biashara ya mtandao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles