23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu awaangukia viongozi wa dini nchini

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Na Mwandishi Wetu, Geita

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa dini kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali  zikiwemo za rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Amesema siku zote  umekuwapo  ushirikiano mzuri kati ya Serikali na asasi mbalimbali yakiwamo madhehebu ya dini katika kuwapatia huduma za  jamii kama vile, afya, elimu, maji, utunzaji wa mazingira na nyingi nyingine.

Majaliwa aliyasema hayo jana alipomuwakilisha  Rais Dk. John Magufuli katika Ibada ya kuwekwa wakfu  na kusimikwa   Mhashamu  Askofu Flavian Kassala kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Geita.

“Serikali inatambua jitihada kubwa zilizowekwa na Kanisa Katoliki katika Jimbo hili la Geita na Tanzania kwa ujumla, hivyo wito wangu kwa Baba Askofu na waumini wa kanisa kwa ujumla wenu ni kuwaomba muendelee na kazi hii nzuri ya kutoa huduma muhimu kwa jamii,” alisema.

Alisema maendeleo ya nchi yanawategemea wote hivyo ushirikiano  kati ya Kanisa na Serikali utawezesha maendeleo ya taifa kupatikana kwa kasi zaidi na kunufaisha wananchi wote.

Jukumu la Serikali ni kuweka mazingira wezeshi ambayo yatasaidia Mtanzania kujikomboa na umaskini na  kazi kubwa ya viongozi wa dini ni kuunganisha jamii na   siyo kuwatenganisha, alisema.

Waziri Mkuu alisema kinachotakiwa kufanywa na wote ni kumwuomba Mwenyezi Mungu awawezesha kuwaelewa viongozi walioko madarakani na kutii maelekezo yanayotolewa kwani hata vitabu vya dini vinaelekeza kutii mamlaka.

Alisema iwapo waumini watatii na kuzingatia mafundisho ya  roho yanayotolewa na viongozi wao wa dini ni dhahiri  yatajenga imani miongoni mwao na upendo utatawala katika jamii nzima.

Waziri Mkuu alisema Serikali itaendelea kushirikiana na madhehebu yote katika kuwahudumia Watanzania wote bila ubaguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles