Ameyasema hayo leo leo Ijumaa Desemba 28, Ikulu jijini Dar es Salaam katika mkutano wake na Shirikisho la Wafanyakazi (TUCTA),Watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya (PSPF na NSSF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA)walipokutana kujadili masuala yahusuyo mafao ya wafanyakazi.
Amesema mifuko hiyo iliunganishwa ili kupunguza gharama za uendeshaji hivyo ni wajibu wa watendaji hao kuhakikisha wanatumia fedha za wanachama kwa ufasaha ikiwamo kupunguza gharama za uendeshaji wa mifuko hiyo
“Wito wangu kwa hifadhi za jamiii zipunguze matumzi ya hovyo, uwekezaji usio na tija usifanyike uwekezaji kama ule ‘Ndege eco village, kule Kigamboni haufai, ule unatakiwa ufanywe na watu binafsi amabao wanajua jinsi ya kulinda fedha zao.
“Huwezi kutumia fedha za wanachama bila ridhaa yao afu baadae uje uwaambie ela hakuna eti ‘formula’ imekataa, sina uhakika kama mlikuwa mnakaa na wafanyakazi mnaamua kuwa mnahitaji hiyo miradi ila watendaji waliopewa dhamana ndo walikuwa waamuzi,” amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amewaagiza watendaji wa mifuko hiyo waanze kutafuta njia bora ya kupata wanachama wapya na katika utafutaji huo ni lazima waweke vipengele ambavyo vitawasaidia wakati wa ulipaji wa mafao.