27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli azitaka PSPF na NSSF kupitia upya daftari la wastaafu

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam Rais John Magufuli amewaagiza watendaji wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii  nchini kupitia upya na kuboresha daftari la wastaafu ili kubaini na kuondoa wastaafu hewa ambao wanalipwa mafao kinyume na sheria.

Ameyasema hayo leo leo Ijumaa Desemba 28, Ikulu jijini Dar es Salaam katika mkutano wake na Shirikisho la Wafanyakazi (TUCTA),Watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya (PSPF na NSSF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA)walipokutana kujadili masuala yahusuyo mafao ya wafanyakazi.

Amesema mifuko hiyo iliunganishwa ili kupunguza gharama za uendeshaji hivyo ni wajibu wa watendaji hao kuhakikisha wanatumia fedha za wanachama kwa ufasaha ikiwamo kupunguza gharama za uendeshaji wa mifuko hiyo

 “Wito wangu kwa hifadhi za jamiii zipunguze matumzi ya hovyo, uwekezaji usio na tija usifanyike uwekezaji kama ule ‘Ndege eco village, kule Kigamboni  haufai, ule unatakiwa ufanywe na watu binafsi amabao wanajua jinsi ya kulinda fedha zao.

“Huwezi kutumia fedha za wanachama bila ridhaa yao afu baadae uje uwaambie ela hakuna eti ‘formula’ imekataa, sina uhakika kama mlikuwa mnakaa na wafanyakazi mnaamua kuwa mnahitaji hiyo miradi ila watendaji waliopewa dhamana ndo walikuwa waamuzi,” amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amewaagiza watendaji wa mifuko hiyo waanze kutafuta njia bora ya kupata wanachama wapya na katika utafutaji huo ni lazima waweke vipengele ambavyo vitawasaidia wakati wa ulipaji wa mafao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles