26.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 7, 2021

Mshirika wa Kenyatta amtaka Ruto astaafu 2022

NAIROBI, KENYA

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama tawala cha Jubilee, David Murathe amesema Naibu Rais William Ruto anatakiwa kustaafu siasa pamoja na Rais Uhuru Kenyatta mwaka 2022.

Mshirika huyo wa karibu wa Kenyatta amesema jamii yao ya Kikuyu haina Hati ya Makubaliano (MoU) na yeyote kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Murathe alitoa kauli hiyo juzi huko Vihiga wakati wa sherehe za kimila za jamii ya Luhya zilizofanyika katika viwanja vya manispaa, Mbale.

Kauli hiyo inaweza kumkasirisha Ruto, ambaye ana matumaini ya kuungwa mkono na Kenyatta atakapostaafu urais mwaka 2022.

Murathe alisema Kenyatta na Ruto wanaongoza serikali kwa mihula miwili na wanapaswa kwa pamoja kustaafu baada ya kutumikia urais na unaibu rais.

Viongozi akiwamo wa chama cha ANC Musalia Mudavadi Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa na kiongzi wa wafanyakazi Francis Atwoli na mamia ya wakazi walisherehekea tukio hilo la kila mwaka ambalo kwa kawaida hufanyika Desemba 26.

“Iwapo William Ruto ana MoU na Uhuru Kenyatta, basi ni makubaliano baina ya watu wawili,” alisema Murathe.

Aliongeza: “Iwapo wewe (Ruto) umeongoza na Uhuru kwa mihula miwili, nini tena unataka. Hatumjui mtu atakayetulinda bali tunamjua mtu atakayetusambaratisha. Tutamchukua mtu atakayehakikisha usalama wa Mlima Kenya.”

Mwanasiasa huyo wa Jubilee, ambaye alishiriki shughuli hiyo ya umma hapo Vihiga kwa mara ya kwanza katika kile kinachoonekaa utayari kufanya ushirika na jamii ya Luhya, alisema chama chao kwa sasa hakina mgombea urais.

Aliendelea kusema hakuna deni lolote kwani Uhuru na Ruto wameongoza serikali kwa usawa.

Alisema ibara 148 (8) ya Katiba inakataza mtu kutumikia unaibu rais kama ilivyo kwa urais kwa mihula miwili.

Hata hivyo, katiba haimzuii Naibu Rais kuwania urais.

Murathe ameonekana kumvalia njuga Ruto kwa kupinga kura ya maoni hata kabla ya chama chao kutoa msimamo

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,400FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles