32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

DC Asia akemea ulevi nyakati za kazi

RAYMOND MINJA- KILOLO

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, Asia Abdallah, amewaonya wananchi wa Kijiji cha Isuka wilayani hapa kwa kuwataka waache utamaduni wa  kunywa pombe wakati wa kazi.

Alisema hatua hiyo hurudisha nyuma maendeleo na hata kusababisha maradhi ya zinaa kwa kufanya ngono zembe kutokana na ulevi.

Hayo aliyasema mwishoni mwa wiki kwenye ziara yake ya kukagua na kusikiliza kero za wananchi kuhusu utendaji wa viongozi wa Serikali kuanzia ngazi ya kijiji hadi halmashauri.

“Ndungu zangu wana-Kilolo hatuwezi kufanikiwa kama tutaendeleza utamaduni wa kunywa pombe wakati wote, kama hawa wenyeviti wangu wa vitongoji wamekunywa pombe mida hii ya saa nne asubuhi, hivi mtaweza kweli kusimamia shughuli za maendeleo, haiwezekani inabidi tubadilike ndugu zangu,” alisema.

Alisema licha ya pombe kufifisha shughuli za maendeleo, lakini pia zimekuwa zikichangia magonjwa ya zinaa kama Ukimwi kwani watu wanapokunywa husahau hata kutumia kinga  na matokeo yake wanafanya ngono zembe na kupata magonjwa  ya zinaa.

“Unajua mkinywa hizi pombe akili huwa  kama imejishoti, hivyo mnavyotoka huko vilabuni wote mmelewa hakuna atakayekumbuka kuvaa kinga, matokeo yake mnafanya ngono zembe mnaambukizana magonjwa  ya zinaa na taifa linakuja kupoteza nguvu kazi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles