20.8 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Polepole wa CCM azitolea uvuvi NGO’s

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humprey Polepole, amesema idadi kubwa ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs) yamepoteza mwelekeo wa kuwahudumia wananchi, hivyo nafasi hiyo inapaswa kuchukuliwa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kusemea na kutatua kero za wananchi.

Kauli hiyo aliitoa mwishoni mwa wiki jijini hapa wakati akifungua mafunzo ya siasa na uenezi kwa makatibu uenezi wa CCM Wilaya ya Dodoma.

“Mimi nilishawahi kuwa kiongozi mkubwa kwenye NGO’s lakini kwa sasa asilimia kubwa ya NGO’s zinapoteza mweleko. Nafasi hiyo inapaswa kuchukuliwa na wana-CCM,” alisema.

Alisema viongozi wa CCM wanapaswa kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia maadili na matendo mema katika kuwatumikia wananchi.

Alisema chama kitaendelea kuwatumikia wananchi na hakitakubali kuyumbishwa na  wapinzani katika kutatua kero za wananchi.

Aidha, aliwataka makatibu uenezi kutotumia lugha za matusi dhidi ya wapinzani, bali wanapaswa kutumia nguvu ya hoja.

“Kiongozi wa CCM kutumia lugha ya matusi ni kwenda kinyume na maadili ya chama. Msiwaite wanachama wa vyama vingine nyumbu,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa, alisema katika uchaguzi mkuu uliopita, walipoteza kata sita ambapo tayari kata nne zimerejea CCM, bado kata mbili ambazo wana uhakika katika uchaguzi mkuu ujao watashinda kwenye kata zote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles