21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Zungu ahamasisha nishati mbadala kulinda mazingira

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu, amehimiza jamii kutumia nishati mbadala ili kupunguza kasi ya matumizi ya mkaa na kuni na kulinda mazingira.

Akizungumza Agosti 18, 2023 wakati wa kukabidhi majiko ya gesi kwa mama na baba lishe, amesema nishati mbadala itapunguza gharama na kuokoa mazingira.

Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu, akizungumza na wafanyabiashara wa Machinga Complex wakati wa kuwakabidhi majiko ya gesi ili kulinda na kuhifadhi mazingira.

Zungu ambaye pia ni Mbunge wa Ilala amegawa majiko 200 kwa mama na baba lishe katika masoko ya Mchikichini, Gerezani na Machinga Complex.

“Rais Samia amejipambanua katika kulinda mazingira, ni muhimu sisi sote tumuunge mkono na tuache kasumba ya kusema chakula kikipikwa kwenye gesi hakiwi kizuri…sikweli chakula kinahitaji moto,” amesema Zungu.

Mmoja wa baba lishe aliyepata jiko hilo Mwishehe Dizeru, amesema mbali ya kulinda mazingira majiko hayo yataokoa gharama walizokuwa wakitumia kununua kuni na mkaa.

“Nilikuwa natumia jiko moja la gesi na moja la mkaa hivyo, kwa kupata jiko hili nitaacha kabisa kutumia mkaa,” amesema Dizeru.

Mama lishe Rukia Milambo amesema majiko hayo yatamrahishia kufanya shughuli zake na kupunguza malalamiko kutoka kwa wateja.

Meneja wa Machinga Complex, Stella Mgumia, amesema matumizi ya kuni na mkaa yanaharibu mazingira na kuhatarisha afya za watumiaji na kuongeza gharama.

“Tunaamini majiko haya yatakwenda kumkomboa mama na baba lishe ambao wanatumia kuni na mkaa. Watapika kwa wakati, kwa usafi na tutatunza mazingira yetu,” amesema Mgumia.

Meneja huyo amewataka wafanyabiashara kwenda kwenye masoko rasmi yaliyotengwa na serikali kwani nafasi zipo na kuna fursa mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles