20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Ziwa Rukwa hatarini kukauka

Ziwa Rukwa
Ziwa Rukwa

Na ELIUD NGONDO, SONGWE

WANANCHI wanaoishi kandokando ya Ziwa Rukwa wilayani Songwe,wametakiwa kupewa elimu ya kuondoa makazi yao ili kunusuru ziwa hilo kukauka.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa wilaya ya Songwe,Samweli Upurukwa wakati wa kikao cha baraza la madiwani kuwa lazima njia mbada itafutwa haraka kunusuru ziwa hilo ambalo limekuwa mkombozi kwa wananchi.

Alisema madiwani wa halmashauri hiyo, wanatakiwa kuwaelimisha wananchi wanaoishi kandokando ya ziwa hilo kuacha kulima na kufanya shughuli zozote za kijamii ndani ya mita 60.

“Madiwani na viongozi wote wa vijiji, vitongoji tunatakiwa kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa ziwa Rukwa,hali ni mbaya na ziwa linaweza kukauka wakati wowote,” alisema Upurukwa.

Kwa upande wake, Mwekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Mbangala, Ibrahim Sambula alisema wananchi hao baada ya kupatiwa elimu wanatakiwa kuondoka ili kupisha uvamizi huo.

Alisema kuna baadhi ya wananchi ambao wamejenga makazi yao pembezoni mwa ziwa hilo ndani ya mita 60 hali ambayo inasababisha kukauka kwa ziwa hilo kila mwaka zaidi ya kilomita mbili.

Alisema wananchi hao wanatakiwa kuondoka mapema,baada ya kupewa elimu ili kuondoa usumbufu wa serikali kutumia nguzu nyingi kuwaondoa maeneo ambayo hawakutakiwa kuwepo.

“Sitakubali kuona mazingira yanaharibiwa na Songwe inabakia kuwa jangwa,wakati ndiko kwenye misitu mingi na hii misitu ndiyo chanzo kikubwa cha kuweza kutuletea mvua,” alisema Upurukwa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Songwe,Elius Nawela alisema wananchi hao wanatakiwa kufuata tarabibu za uhifadhi wa mazingira ilikuweza kuokoa kukauka kwa ziwa hilo.

Alisema ziwa hilo linakauka kutokana na shughuri za kibinadamu ambayo zimekuwa zikifanyika kila kuangalia matatizo ya miaka ijayo, hivyo kuwepo kwa utoaji wa elimu hiyo na katazo likatolewa itakuwa ni tija ya kunusuru ziwa hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles