Clinton amtuhumu Trump kununua wahuni kumzomea

0
652
MGOMBEA urais kupitia Chama cha Democrat, Hillary Clinton
MGOMBEA urais kupitia Chama cha Democrat, Hillary Clinton
MGOMBEA urais kupitia Chama cha Democrat, Hillary Clinton

NA JUSTIN DAMIAN, MAREKANI

MGOMBEA urais kupitia Chama cha Democrat, Hillary Clinton, jana uzalendo ulimshinda na kuwakemea waandamanaji waliokuwa wakimzomea katika mkutano wake wa kampeni, huku akimtuhumu hasimu wake, Donald Trump kuwatuma.

Waandamanaji hao waliokuwa wamebeba mabango yaliyosomeka ‘Bill Clinton ni mbakaji’ katika jimbo la Florida, walimpa usumbufu mkubwa mgombea huyo wakati akihutubia kutokana na kelele na maneno waliyokuwa wanayatoa.

Akiwa kwenye mkutano huo wa hadhara, Clinton alionyesha waziwazi kukerwa na kitendo cha waandamanaji hao na kumshutumu Trump kufadhili vitendo visivyo vya kiungwana katika kampeni.

“Nimechoshwa na vitendo vya giza na uchokozi vinavyotoa picha mbaya ambavyo vinafanywa na wafuasi wanaomuunga mkono Donald Trump,” alisema Clinton kwa sauti yenye hasira.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here