27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Zitto Kabwe kupanda kizimbani leo

TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM



KESI ya jinai namba 367 ya mwaka 2018 inayomkabili Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe itaendelea leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini, anakabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la uchochezi na kutoa taarifa za uongo kuhusu mauaji ya baadhi ya askari polisi na wananchi katika Kijiji cha Mpeta, wilayani Uvinza mkoa wa Kigoma.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu alisema wananchi wafuatilie habari hiyo kupitia vyombo vya habari na waliopo katika jiji la Dar es Salaam wafike mahakamani.

“Tunapenda kuwataarifu wananchi na wanachama wetu kuwa kesi inayomkabili Zitto itaendelea kesho hivyo tunawaomba tukutane Kisutu,” alisema Shaibu.

Alisema wanawashukuru wote waliosaidia kutoa shinikizo lililosaidia kumwachia huru ama kumpeleka mahakamani.

“Tunaamini kuwa shinikizo hilo ndilo lililosababisha Jeshi la Polisi kumpeleka kiongozi wetu mahakamani na kupata dhamana,” alisema Shaibu.

Shaibu alisema kitendo cha viongozi wa vyama vya siasa kuwa na kesi mahakamani kimeunganisha vyama vyote vya upinzani na kuondosha tofauti zao.

“Hizi kesi kadri zinavyoendelea zinatuleta pamoja tunatoa salamu za kimshikamano kwa wenzetu tuko pamoja nao katika kesi zao  CUF  na Chadema,” alisema Shaibu.

Akizungumzia suala la uvuvi Shaibu aliitaka Serikali kuwashirikisha wavuvi kwenye utungaji wa sheria, kanuni na makato pia kwenye programu zake hasa zinazowagusa wavuvi moja kwa moja ili kujua mahitaji yao.

Alisema Serikali ihakikishe inapofanya operesheni kukabiliana na uvuvi haramu wasiteketeze zana zingine ambazo si haramu kama vile mitumbwi ya wavuvi.

“Tunawaomba wavuvi watoe ushirikiano kwa serikali katika kuwabaini wanaojihusisha na uvuvi  haramu  kwakuwa maziwa na bahari vikibaki bila samaki hata wavuvi hawatakuwapo,” alisema Shaibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles