22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Z’bar yaanza kutumia teknolojia ya kupimia Corona

Na KHAMIS SHARIF-ZANZIBAR

WIZARA ya Afya Zanzibar imeanza kutoa huduma za uchunguzi wa virusi vya maradhi ya Covid -19 kwa wananchi na wageni wanaoingia nchini kwa kutumia mashine maalum ya kuchunguzia maradhi ya mripuko.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Huduma za Uchunguzi wa Maradhi katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dk. Msafiri Marijani amesema kifaa hicho kina uwezo wa kuchunguza zaidi ya sampuli 90 kwa wakati mmoja na kutoa majibu ndani ya masaa 24.

Alisema wizara tayari imeshatoa mafunzo kwa wafanyakazi sita  kutoka kwa wataalamu walioleta mashine hiyo kwa ajili ya matumizi ya kifaa hicho hadi sasa imeshachunguza sampuli 260 na kutoa majibu sahihi.

“Serikali imeamua kuingia teknolojia hii ili kukabiliana na matatizo mbalimbali ya kibinaadamu ikiwe hili za Corona ambalo linaisumbua dunia na kuathiri maisha ya watu na kupoteza maisha ya watu, hii ni mashine ambayo ina uwezo mkubwa kimatumizi na tutahakikisha kunaitumia ipaswavyo,” alisema mkurugenzi huyo.

Dk. Marijani alisema mashine hiyo pia itasaidia kuchunguza maradhi mbali mbali ya mripuko ikiwemo ebola na 

chikungunya ikiwa  yatatokezea nchini

Aidha aliishukuru Serikali na washirika wa maendeleo nchini akiwemo mfanyabiashara Rostam Azizi kwa kusaidia  kifaa hicho cha kupunguza usumbufu wa kupeleka sampuli nje ya Zanzibar.

Kifaa hicho kiliwasili nchini mwezi Mei mwaka huu kutokana na kuingia kwa mripuko wa maradhi ya Corona-19 na kuanza kutumika Oktoba mwaka huu. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles