25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

ZARI AMTWANGA SWALI MAMA DIAMOND

Na MWANDISHI WETU

BAADA ya mkali wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond Platinumz’, kufunguka kuwa mtoto wa mwanamitindo, Hamisa Mobeto, Abdul ni wake, mzazi mwenzake, Zarina ‘Zari’ Hassan, ameibuka na kumpiga swali zito mama wa msanii huyo, Sanura Kassim.

Zari maarufu kama The Boss Lady, alitumia akaunti yake ya Instagram kumuuliza mama mkwe wake huyo kuhusu ahadi yake ya umama kwake baada ya dada huyo wa Uganda kufiwa na mama yake mzazi, Halima Hassan.

“Mama Dangote (Mama Diamond), hii ahadi ya umama kaiua Dangote au?” Katika akaunti hiyo aliambatanisha picha na kile ambacho aliwahi kukiandika mama yake Diamond kwenye akaunti yake ya Instagram baada ya Zari kufiwa.

Mama yake Diamond, aliandika: “Umepoteza mama na umebaki na mama ambaye ni mimi, mama Latifa tumshukuru Mungu kwa kila hali.”

Kauli hiyo ndiyo imemfanya Zari ahoji umama wa mama yake Diamond kwake, baada ya msanii huyo kumsaliti mzazi mwenzake huyo ambaye amezaa naye watoto wawili na kwenda kuzaa na Hamisa.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles