26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Zaidi ya watoto milioni tano wapatiwa vyeti vya kuzaliwa

Asha Bani-Dar es salaam

Serikali kupitia Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), umefanikisha kusajili watoto wa umri chini ya miaka mitano zaidi ya milioni tano na kupata vyeti vya kuzaliwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa usajili matukio muhimu ya binadamu.

Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Emmy Hudson ambapo amesema mpango wa usajili wa watoto una lengo la kuhakikisha kila mtoto aliye na umri chini ya miaka mitano anasajiliwa na kupata cheti cha kuzaliwa.

“Kila mtoto anayezaliwa anapata nyaraka hiyo ndani ya muda mfupi baada ya tukio la kizazi kutokea, utekelezaji wa mpango huu unafanyika kwa kusogeza huduma karibu na makazi ya wananchi kwa kutoa huduma bila malipo katika ofisi za watendaji kata na vituo vya tiba vinavyotoa huduma ya afya ya mama na mtoto,’’alisema Emmy.

Ameongeza kuwa wamekuwa na mafanikio ambapo zaidi ya watoto milioni 5 wamesajiliwa na kupata vyeti mpango uliofanyika katika mikoa ya 18 ambayo mpango huu unatekelezwa na idadi hiyo kuweza kupandisha wastani wa watoto walio na vyeti vya kuzaliwa kutoka asilimia 13 na sasa kufikia asilimia 49.

Amesema kati ya watoto waliosajiliwa asilimia 50.1 ni wanaume na asilimia 49 ni wanawake ambapo mikoa 18 imefikiwa kwa huduma hiyo.

Aliitaja mikoa hiyo ni pamoja na Mbeya, Songwe, Mwanza, Iringa, Njombe, Geita, Shinyanga, Mtwara na Lindi.

Mikoa mingine ni pamoja na Mara, Simiyu, Ruvuma, Dodoma, Singida, Morogoro, Pwani, Tanga na Kilimanjaro.

“Mpango wa Usajili wa watoto ulianza kutekelezwa mwaka 2013 huku kasi ya usajili ikiwa ni ndogo wakatio huo na kasi imeongezeka katika kipindi cha serikali ya awamu ya tano na katika kipindi cha miaka mitano ambapo mfumo umesimikwa na kuanza kutekelezwa katika mikoa 15 na zaidi ya watoto 4,051,186 wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa,’’alieleza Emmy.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles