26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mkuu wa Wilaya Bariadi atangaza bei mpya ya pamba kwenye wilaya yake

Derick Milton, Simiyu

Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga ametangaza bei mpya ya kununulia zao la pamba kutoka kwa wakulima ambayo inatakiwa kufuatwa na wanunuzi wote wanaonunua zao hilo kwenye wilaya yake kuwa ni Sh.900 kwa kilo moja.

Kiswaga ametangaza bei hiyo mpya kutoka bei elekezi ya serikali ambayo ilitangazwa na Bodi ya Pamba kabla ya kuanza kwa msimu wa ununuzi wa zao hilo Sh.810.

Akitangaza uhamuzi huo leo mara baada ya kuendesha mnada katika kata ya Nkololo wilayani humo mbele ya wakulima na Kampuni tatu za Alliance ginnery, Olam Ltd na Birchald ambazo and zinazonunua pamba wilayani humo.

Katika mnada huo Kampuni zote tatu zilishindana kutangaza bei, ambapo Kampuni ya Alliance ilitangaza kununua pamba kwa sh. 910 huku nyingine zikuitangaza kununua kwa sh.900.

“Kuanzia sasa katika wilaya yangu ya Bariadi zao la pamba litanunuliwa kwa sh. 900 kwa kilo moja na kuendelea, na makampuni haya matatu ndiyo yatanunua, bei imepanda na makampuni yenyewe ndiyo yamepandisha, kwa hiyo kwa wilaya hii bei ni sh.900” amesema Kiswaga.

John Kabole ambaye ni oparesheni kutoka kampuni ya Allinace ginnery amesema wao kama kampuni ya ununuzi wa pamba wako tayari kununulia pamba kwa bei ya shilingi 900 kama ilivyotangazwa na Mkuu wa Wilaya.

Nsiya Ludaya mkulima na mkazi wa kitongoji cha Isanga-Nkololo alimpongeza mkuu wa wilaya hiyo kusimamia ununuzi wa pamba ikiwemo kuendesha mnada ambao umepandisha bei ya zao hilo kutoka shilingi 810 waliyokuwa wakinunuliwa awali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles