SERIKALI ya Uturuki imesema imezifunga zaidi ya taasisi 2000 zenye uhusiano na kiongozi wa dini anayeishi Marekani, Fethullah Gulen, ambaye anashitakiwa kwa kupanga mapinduzi ya kijeshi yaliyoshindwa, Julai 15 mwaka huu.
Mashirika yaliyofungwa ni pamoja na vituo vya afya na zaidi ya shule binafsi 1000.
Serikali ya Uturuki inazituhumu a taasisi hizo kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na Gulen ambaye ana wafuasi wengi nchini humo.
Habari zinasema hatua hizo zimechukuliwa kama moja ya jitihada kubwa za kukabiliana na mitandao inayomuunga mkono Gulen.
Gulen amekwisha kukanusha kuhusika na njama za mapinduzi ya jeshi nchini humo yaliyosababisha vifo vya watu wapatao 246.
Maelfu ya wanajeshi, polisi na watu wengine wanaendelea kukamatwa nchini Uturuki kutokana na jaribio la mapinduzi