Msumbiji
Serikali ya Msumbiji imesema inahitaji zaidi ya dola za Marekani milioni 114 sawa na pauni milioni 82 kwa ajili ya ujenzi mpya wa mji wa kaskazini wa Palma, ulio katika jimbo la Cabo Delgado, ambao hivi karibuni uliharibiwa na magaidi wa kiislamu.
Waziri wa utawala wa nchi na huduma za Umma Ana Comoana ameeleza hali ilivyo katika mji wa Palma kuwa ngumu sana, yenye kushtua na yenye vurugu.
Waziri huyo amesema miundombinu na rasilimali fedha vimeharibiwa kwenye shambulio pia ameongezea na kusema serikali inapaswa kujiandaa kuujenga upya mji huo, lakini hakusema ni kwa namna gani fedha zitapatikana kwa ajili ya azma hiyo.