23.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 26, 2021

Watu 7 wauawa na 22 kujeruhiwa dhidi ya maandamano nchini Congo

DR congo

Maandamano yanayoendelea  wilaya ya nyiragongo jimbo la Kivu kaskazini mashariki mwa Kongo yamesababisha vifo vya watu 7 na wengine 22 kujeruhiwa.

Maandamano hayo yaliyoanza wiki iliyopita katika miji ya Beni, Butembo na Goma wakitaka kuondolewa kwa vikosi vya UN kwa madai ya kushindwa kudhibiti makundi ya magaidi wanaendelea kuua watu nchini humo.

Waziri wa ulinzi jimboni humo, Bosco Sebishyimbo amesema Mapigano yalianza Jumatatu baada ya watu wawili wa kabila la Kumu kukutwa wamekufa huku mauaji hayo yakidaiwa kufanywa na watu wa kabila la Nande.

Pia taarifa zinasema nyumba kadhaa zimeteketea kwa moto , katika mapigano kati ya kundi la waandamanaji na polisi Jumatatu katika mkoa wa Bukumu, eneo la Nyiragongo .

Gavana wa Jimbo la Kivu kaskazini Carly Kasivita amethibitisha hayo hii leo na kusema kwamba idadi ya waliopoteza maisha huenda ikaongezeka

Katika miji ya Beni, Butembo na Goma kumekuwa na maandamano ya hivi karibuni dhidi ya mauaji na ukatili unaofanywa na vikundi vyenye silaha huko Beni na eneo hilo lina makazi ya walinda amani wengi wa UN.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,190FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles