27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

YOUNG DEE AFUNGUKA PICHA ZA UTUPU NA AMBER LULU

NA CHRISTOPHER MSEKENA

WIKI hii zilivuja picha zikiwawonyesha staa wa ngoma ya Bongo Bahati Mbaya, Young Dee akiwa na video vixen, Amber Lulu wakiwa kihasarahasara ambazo kila mmoja hafahamu nani amezivujisha licha ya kukiri kuwa wanafahamu siku zilipopigwa.

Young Dee ambaye hivi sasa anajiandaa kuachia ngoma mpya ameiambia ShowBiz, kuwa anawaomba radhi mashabiki wake waliochukizwa na picha hizo na tayari amechukua hatua kwa kutoa taarifa polisi kwa ajili ya kumbaini aliyezivujisha.

“Nimesikitishwa na hizo picha sababu zinaniharibia image yangu kwa mashabiki ambao toka kitambo wananisapoti… ile picha ilipigwa nyuma ya kamera wakati tunapiga picha za nguo mpya za ki-scottish zinazofanana na sketi, hazikuwa kwa lengo la kuzitoa,” alisema Young Dee na kusisitiza:

“Sheria itachukua mkondo wake kwa aliyezivujisha, maana tayari ishu hiyo ipo mikononi mwa polisi ambao wanaendelea na uchunguzi. Kuna mtu amefanya uhuni.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles