20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga: Zutah bado ni mali yetu

zuttaNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya Yanga umesema beki wa kimataifa wa timu hiyo, Joseph Zutah, bado ni mali yao halali licha ya kuwa jina lake halipo katika orodha ya wachezaji iliyowasilishwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Jonas Tibohora, alisema jina la Zutah halipo kwenye orodha ya wachezaji watakaocheza msimu mpya wa Ligi Kuu lakini wana mipango ya muda mrefu na mchezaji huyo.

Tibohora alisema mpango wao kwa mchezaji huyo raia wa Ghana, utawashangaza mashabiki na wadau wengi wa soka hapa nyumbani.

“Tuna mipango yetu kama uongozi, kukosekana kwa jina la mchezaji huyo katika idadi iliyowasilishwa TFF siyo sababu ya kuachana naye,” alisema Tibohora.

Katibu huyo alieleza wana imani mipango yao itakuwa gumzo kwa kila mtu na itaongeza heshima ya klabu hiyo, itakayotetea ubingwa wa ligi msimu ujao.

“Zutah ataendelea kuonekana akifanya mazoezi kama kawaida, ingawa kwenye mechi za ligi hatoweza kushiriki lakini mwalimu ataendelea kumfundisha,” alisema Tibohora.

Alieleza kuwa hawajavunja mkataba na mchezaji huyo, hivyo wanamtambua kama ni wao na hata Zutah mwenyewe analifahamu hilo.

Zutah alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo, kabla tetesi za uongozi wa klabu kuvunja mkataba huo kwa madai ya kutoridhishwa na kiwango chake.

Mchezaji huyo alikuwa benchi wakati kikosi hicho kikivaana na Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Agosti 22 mwaka huu, ambapo kwenye  mazoezi yaliyofanyika jana hakuweza kuhudhuria kutokana na kuugua malaria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles