29.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yakiri Tuisila kuondoka

Na WINFRIDA MTOI, Mtanzania Digital

UONGOZI wa klabu ya Yanga umekiri kuwa mchezaji wake Tuisila Kisinda, amepata ofa kubwa nchini Morocco hivyo hatakuwa katika kikosi cha msimu ujao,akidaiwa kutimikia timu ya RS Berkane inayonolewa na kocha wake wa zamani AS Vita Club Florent Ibenge. 

Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Haji Mfikirwa, amesema ofa walioyopta hawawezi kuikataa kwa maslahi ya mchezaji na klabu pia.

Amesema kutokana na hilo wapo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mchezaji atakayeziba pengo lake.

“Ni kweli Tuisila   tulipokea ofa kutoka Morocco, wakihitaji huduma yake kwa faida ya mchezaji tunamruhu aondoke kwa sababu na Yanga pia itapata faida kubwa katika ofa hiyo.

“Huu ni wakati wake sahihi na sisi tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa mbadala wake”, amesema Mfikirwa.

Nyota huyo aliyesajiliwa msimu uliopita, alikuwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Wanajangwani hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles