28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Aucho afunguka kilichompeleka Jangwani

Na WINFRIDA MTOI, Mtanzania Digital

Baada ya kutambulishwa rasmi leo, kiungo mpya wa Yanga Mganda, Khalid Aucho, amesema amejiunga na timu hiyo akiamini ni sehemu atakayocheza soka kwa furaha na kujiamini kwa sababu ni kama familia yake.

Akizungumza wakati akitambulishwa, Aucho, amesema kuna timu nyingi zilikuwa zikimhitaji ambazo zimepitia kwa wakala wake lakini Yanga walimuendea hewani mwenyewe.

Amesema ana mapenzi na Yanga, pia wakati wanamfuatilia alikuwa akizungumza vizuri na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Hersi Said  ambaye ni kama mwanafamilia  kwake.

“Nimekuja Yanga kwa mapenzi yangu na timu, waliongea na mimi mwenyewe kama mwanafamilia, lakini timu nyingine zilipitia kwa wakala,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles