Na WINFRIDA MTOI, Mtanzania Digital
UONGOZI wa klabu ya Yanga umekiri kuwa mchezaji wake Tuisila Kisinda, amepata ofa kubwa nchini Morocco hivyo hatakuwa katika kikosi cha msimu ujao,akidaiwa kutimikia timu ya RS Berkane inayonolewa na kocha wake wa zamani AS Vita Club Florent Ibenge.
Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Haji Mfikirwa, amesema ofa walioyopta hawawezi kuikataa kwa maslahi ya mchezaji na klabu pia.
Amesema kutokana na hilo wapo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mchezaji atakayeziba pengo lake.
“Ni kweli Tuisila tulipokea ofa kutoka Morocco, wakihitaji huduma yake kwa faida ya mchezaji tunamruhu aondoke kwa sababu na Yanga pia itapata faida kubwa katika ofa hiyo.
“Huu ni wakati wake sahihi na sisi tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa mbadala wake”, amesema Mfikirwa.
Nyota huyo aliyesajiliwa msimu uliopita, alikuwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Wanajangwani hao.