24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga: Ngassa kila la heri

Pg 32, NgassaNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM
UONGOZI wa Klabu ya Yanga umemtakia kila la heri aliyekuwa mchezaji wao, Mrisho Ngassa, baada ya kupata ulaji nchini Afrika Kusini.
Ngassa jana ameingia mkataba wa miaka minne kuichezea timu Free State Stars, inayocheza Ligi Kuu nchini humo, baada ya kufuzu majaribio na kukabidhiwa jezi rasmi.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha, alisema ni jambo la kujivunia kwa klabu kutoa mchezaji kucheza soka la kulipwa la kimataifa na wamefurahi sana kwa kufuzu majaribio hadi kuchukuliwa.
“Ngassa alikuwa tayari amemaliza mkataba kuichezea Yanga baada ya ligi kumalizika, hivyo tumefurahishwa na ulaji huo mnono alioupata na tunamtakia kila la heri,” alisema.
Kwa mujibu wa mtandao wa Bin Zubeiry, Ngassa ameonyesha kufurahishwa na timu hiyo na kudai kuwa hiyo ni changamoto mpya kwenye maisha yake na atatumia fursa hiyo kuweza kuitangaza nchi yake kwa kuonyesha kiwango cha juu.
“Sasa najiandaa kwa maisha mapya baada ya kucheza Tanzania kwa muda mrefu, hii ni changamoto mpya kwangu, mpira wa Afrika Kusini upo juu sana ukilinganisha na nyumbani. Nataka kutumia fursa hii kulitangaza soka la Tanzania, ili kuzivuta klabu nyingine kusajili wachezaji wa nchini kwetu,” alisema.

Wakati huo huo, winga Geodfrey Mwasuya kutoka timu ya Kimondo Mbeya jana amesaini mkataba wa miaka miatatu kuitumikia Yanga, ambapo ataridhi mikoba ya Ngassa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles