23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga kuweka kambi A.Kusini

yangaWINFRIDA NGONYANI NA ADAM MKWEPU, DAR

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wanatarajia kuweka kambi ya muda mfupi nchini Afrika Kusini kujiandaa na mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria ugenini.

Yanga ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa, wanatarajia kuondoka nchini Ijumaa wiki hii kuelekea Afrika Kusini kwa ndege ya Shirika la South Africa baada ya wachezaji kumaliza mapumziko ya wiki moja.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, alisema timu hiyo itarejea mapema kwa ajili ya kucheza mechi moja ya kujipima nguvu kabla ya kukutana na Mo Bejaia ugenini.

“Tumechagua kuweka kambi ya muda mfupi Afrika Kusini kutokana na hali ya baridi iliyopo nchini humo ili wachezaji waweze kuizoea tutakaposafiri kwenda Algeria kuwakabili wapinzani wetu Mo Bejaia,” alisema Muro.

Yanga itaanza kampeni yake ugenini dhidi ya Mo Bejaia Juni 17 kabla ya kuwa mwenyeji wa TP Mazembe Juni 28 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizia mzunguko wa kwanza nyumbani dhidi ya Medeama ya Ghana Julai 15, mwaka huu.

Wakati huo huo, uongozi wa klabu ya Yanga umeanza kuandaa mikakati ya kuwafanyia ‘ushushushu’ wapinzani wao Mo Bejaia kabla ya kuwakabili katika mchezo wa kwanza wa Kundi A.

Ili kufanikisha mipango hiyo, viongozi wa Yanga wamepanga kukutana Mei 30 (leo) na Juni 6, mwaka huu ili kujadili mbinu zitakazowawesha kupata ushindi dhidi wapinzani wao.

Chanzo cha habari za uhakika ambazo MTANZANIA lilizipata jana, kilieleza kuwa msingi wa kikao hicho ni kutaka kujadili njia watakazotumia kupata kanda za video za michezo iliyopita ya Mo Bejaia na pia kujiweka tayari kukabiliana na mbinu za hujuma ambazo zinaweza kufanywa na Waarabu hao.

“Kwa sasa tupo kwenye mapumziko ya muda mfupi lakini kesho (leo) na Juni 6, mwaka huu tutafanya kikao kitakachotuwesha kuibuka na ushindi ugenini dhidi ya Mo Bejaia, ambapo pia wachezaji waliopo kwenye timu za Taifa watakuwa wamerudi.

“Pia tutajadili kuhusu maandalizi ya kambi kwa wachezaji kabla ya kucheza mechi hiyo ya kwanza ya hatua ya makundi,” kilieleza chanzo hicho.

Wachezaji wa Yanga walioitwa kwenye timu za taifa ni Vincent Bossou (Togo), Haruna Niyonzima (Rwanda), Deogratius Munishi ‘Dida’,  Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Kelvin Yondani na Deus Kaseke (Taifa Stars).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles