31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Bilal awaasa vijana

Dk. Mohamed BilalNA FARAJA MASINDE, DAR ES SALAAM

MAKAMU wa Rais mstaafu, Dk. Mohamed Bilal, amewaasa vijana akiwataka kujenga utamaduni wa kujifunza lugha mbalimbali ili kujijengea mazingira rahisi ya ajira.

Hayo aliyasema   Dar es Salaam juzi kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Lugha na Utamaduni (IFCL).

Alisema   kutokana na kuwapo  changamoto kubwa ya ajira vijana hawana budi kujifunza lugha nyingi za kigeni kwa ajili ya kuwasaidia.

“Ni heshima kubwa kuona kuwa Tanzania imepata fursa kubwa ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho haya ambayo yamejumhisha mataifa 30.

“ni wajibu kwa vijana kuanza sasa kujifunza lugha nyingine za kigeni kwa ajili ya kusaidia kupambana na ushindani uliopo kwenye soko la ajira ikizingatiwa  dunia hii tuliyo nayo sasa hivi ukijua lugha nyingi za kigeni unakuwa na faida kubwa kuliko yule anayejua lugha moja.

“Napenda nitoe wito kwa mataifa yote kuendelea kutumia maadhimisho haya kama njia ya kujenga umoja na mshikamano ili kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi.

|Lakini pia hii ni fursa nzuri kama nchi kuendelea kuboresha uhusiano wetu na mataifa mengine jambo ambalo litajenga vijana kuwa mabalozi wazuri kupitia lugha na utamaduni ,” alisema Dk. Bilal.

Alisema kwa kwa sasa dunia imekuwa ikipitia kwenye misuguano ya siasa ambayo inasababisha  machafuko  na  viongozi mbalimbali wanatumia maadhimisho hayo kujenga ushirikiano na umoja.

“Kama Tanzania ambayo tunatarajia kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025, hivyo ni wazi kuwa vijana hawa watakuwa ni moja ya daraja la kuboresha ushirikiano na maendeleo ya uchumi kupitia kujifunza mambo tofauti kutoka kwenye mataifa mengine, ” alisema

Naye Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute(KDI), Ali Akkiz,  alisema maadhimisho hayo yaliwakutanisha vijana kutoka nchi 30.

“Kila nchi imetoa mwanafunzi mmoja na mwalimu wake, mbali na maonyesho haya pia wanafunzi watapata fursa ya kutembelea kwenye vituo vya watoto yatima na vivutio vya utalii   nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles