25.4 C
Dar es Salaam
Thursday, January 9, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Yanga hakuna kulala

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KIKOSI cha Yanga, kimetua nchini kikitokea Botswana na kuingia moja kwa moja kambini kujiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga walikuwa Botswana kuikabili Township Rollers ya huko katika mchezo wa marudiano wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers na kupata ushindi wa bao 1-0.

Ushindi huo umeiwezesha timu hiyo kusonga mbele katika michuano hiyo kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1, ikiwa ni baada ya sare ya bao 1-1 waliyoipata dhidi ya wapinzani wao hao kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wiki mbili zilizopita.

Wanajangwani hao walirejea nchini usiku wa kuamkia jana na jioni yake kuendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh, alisema hawawezi kupumzika ukizingatia wanakabiliwa na mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.

“Tuliingia usiku wa kuamkia leo (jana) na jioni tutaendelea na mazoezi katika Uwanja wa Polisi, hivyo hakuna kupumzika, ukizingatia ligi ndio imeanza, lazima tuwe makini,” alisema.

Alisema kikosi chote kipo vizuri kukiwa hakuna majeruhi na kwamba kila mchezaji morali ipo juu kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo na kuanza ligi kwa ushindi.

Yanga ilipokutana na Ruvu Shooting msimu uliopita, mzunguko ilishinda mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Taifa, kabla ya kupata ushindi wa bao 1-0 waliporudiana katika dimba hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles