32.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Yajayo Bwawa la Nyerere yanafurahisha

*Ni baada ya kina cha maji kufikia kiwango kinachohitajika

*Utekelezaji wake wafikia asilimia 90

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wizara ya Nishati imeeleza kuwa ndani ya wiki moja iliyopita imefanikiwa kujaza maji kwa kiwango kinachotosheleza uzalishaji umeme katika Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Julias Nyerere (JNHPP).

Waziri wa Nishati, Januari Makamba akizungumza na Waandishi wa Habari.

Ikumbukwe kuwa, kina cha bwawa lote ni mita 184 kutoka usawa wa bahari, hata hivyo kiwango kinachotakiwa kufikiwa ili kuzalisha umeme ni ni mita 163 kutoka usawa wa bahari na kwamba hadi kufikia jana Julai 5, 2023 bwawa hilo lilikuwa limefikia mita 163.61.

Akizungumza mapema leo Julai 6, 2023 jijini Dar es Salaam Waziri wa Nishati, Januari Makamba ambapo amesema kuwa hadi sasa mradi huo unaendelea vizuri na kwa kasi ya hali ya juu ambapo hadi sasa umefikia asilimia asilimia 90 ya utekelezaji wake.

“Huko nyuma kumekuwa na hofu kubwa ya kwamba je, maji yatajaa kuweza kuzalisha umeme katika bwawa hilo, tulikadiria tutakuwa na misimu mitatu ambayo ndiyo itatosheleza kujaza bwawa hilo lakini ndani ya msimu mmoja wiki iliyopita Wizara ya Nishati imefanikiwa kujaza maji kwa kiwango kinachotosheleza kuzalisha umeme kwenye bwawa hili la Mwalimu Nyerere,” amesema Makamba.

Aidha, Makamba amesema kazi ya ufungaji mitambo inaendelea na kufikia Februari, mwakani tutaanza majaribio ya kuzungusha mitambo kwa maji.

“Kwa lugha rahisi ni kwamba kufikia Juni, 2024 tutaanza kutoa umeme pale Mwalimu Nyerere na kuuingiza katikia gridi ya taifa,” amesema Majkamba na kuongeza kuwa:

“Kuhusu ujazo wa maji, bwawa hilo limefikia lita za ujazo bilioni 30, mpaka Julai 5, mwaka huu. Maji yaliyoingia mle ndani ni mita za ujazo bilioni 13. 8 ambazo ni sawa na asilimia 43,” amesema.

Kuhusu Bomba la Mafuta

Mbali na hayo Makamba amesema Wizara ya Nishati itafanya kikao kazi cha Mawaziri kutoka Tanzania na Zambia kitakachojadili ushirikiano baina ya nchi hizo mbili juu ya ulinzi na usalama katika ulinzi na usalama wa bomba la mafuta la TAZAMA na sekta ya nishati kwa ujumla wake.

Amesema katika kinao hicho watatathimini utekelezaji wa masuala ya ulinzi na usalama wa bomba la mafuta la TAZAMA kama ilivyokubalika katika kikao cha kwanza cha wizara hizo tatu kilichofanyika Desemba, 2022 jijini Dar es Salaam baada ya Serikali ya Zambia kuamua kutumia bomba hilo kusafirisha mafuta safi badala ya mafuta ghafi.

“Tutapokea taarifa mapendekezo ya ujenzi wa bomba jipya, bomba hili lilijengwa muda mrefu na lina kipenyo chembamba, kwasababu biashara imekua na mahitaji ya mafuta yameongezeka imeonekana kwamba kuna haja ya kujenga bomba pana zaidi litakaloweza kusafirisha pia bidhaa nyingine zaidi ya dizeli,” amesema Makamba na kuongeza kuwa:

“Bomba la TAZAMA lina urefu wa Km 1.710 kutoka Kigamboni-Dar es Salaam hadi Indeni -Ndola, Zambia, changamoto kubwa ni ulinzi na usalama wa bomba hili baada ya kuanza kusafirisha mafuta yaliyosafishwa badala ya mafuta ghafi.

“Bomba hili sasa hivi linasafirisha takribani lita milioni 90 kwa mwezi, hivyo kama litakuwa na ufasini, wenzetu wa Zambia wataendelea kuitegemea Bandari yetu ya Dar es Salaam kuingizia mafuta nchini mwao na tukijenga bomba kubwa zaidi, pia bandari ya Dar es Salaam itapata soko kubwa zaidi kwa ajili ya mafuta yanayokwenda Zambia na hatimaye kwenda Kongo,” amesema Makamba.

Amesisitiza kuwa ufanisi wa bomba hilo utasaidia la TAZAMA kupunguza gharama za usafirishaji wa mafuta na kuweza kuisaidia mikoa ya Kusini mwa Tanzania kupata mafuta kwa unafuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles