29.7 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania watakiwa kushiriki udhibiti dawa za kulevya

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Katika kuhakikisha kuwa matumizi ya dawa za kulevya nchini yanadhibitiwa, jamii imeaswa kuelimisha watoto na vijana juu ya athari zitokanazo na matumizi ya dawa hizo ili kuwa na taifa imara hapo baadaye.

Hayo yamebainishwa Julai 6, jijini Dar es Salaam na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kuapamana na dawa za kulevya nchini Tanzania (DCEA), Aretas Lyimo alipotembelea banda la mamlaka hiyo katika maonyesho ya Sabasaba.

Amesema mkakatiwa Serikali ni kuhakikisha kuwa matumizi ya dawa hizo yanabaki kuwa historia huku wale walioathirika nadawa hizo wakiwezeshwa kiuchumi.

“Jamii ya Watanzania bado haitambui jukumu lao katika kuelimisha watoto athari za matumizi ya dawa wa kulevya na wazazi wengi hawachukui majukumu yao kumlinda mtoto au kijana, wanapaswa kutambua kuwa jukumu hili ni la kila mmoja wetu kuanzia ngaiz ya chini hadi taifa,” amesema Kamishina Jenerali Lyimo.

Amesema ongezeko kubwa la matumizi ya dawa zza kulevya Serikali inampango wa kufanya utafiti wa maeneo yanayolima bangi na mirungi ili kubadilisha kilimo hicho na kuwawezesha wakulima hao kulima kilimo mbadala kitakachokuwa na tija na kuwanufaisha

“Asilimia 10 ya mikopo inayotolea na Halmashauri nchini inatolewa kwa vijana lengo likiwa ni wao kujiendeleza na kuacha kukaa vijiweni na kushawishika kuingia kwenye makundi yanayochochea wao kuingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya,” amesema.

Katika hatua nyingine amefafanua kuwa, kiasi kikubwa wanaoingia katika dawa za kulevya ni wanafunzi na watoto ambao wapo mtaani na kwamba wao kwa kuliona hilo wanatoa elimu na kuanzisha Klabu za dawa za kulevya atika shule na vyuo nchini ili kujenga uelewa kwa wanafunzi kuhusu athari za matumizi ya dawa hizo.

“Uwepo wetu kwenye maonyesho haya ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu athari za matumizi ya madawa ya kulevya lakini pia wananchi kutufamu sisi na shughuli zetu,” ameongeza.

Amesema elimu nzuri kuhusu athari zinazotokana na madawa ya kulevya inapaswa ianzie nyumbani tangu mtoto akiwa mdogo hatua ambayo itamjenga na kumsaidia kuogopa kufanya biashara hiyo na kutumia.

Kamishina Jenerali Lyimo ametaja mikoa iliyobainika kulimwa bangi kwa wingi nchini kuwa ni Arusha, Mara na Morogoro huku Kilimanjaro ikilima mirungi kwa wingi hivyo utafiti utaanza kwenye maeneo hayo ili kuwekewa miundombinu rafiki ya kilimo mbadala.

Ametoa wito kwa wazazi kuwaleta watoto kwenye maadili na kuwapa elimu juu ya athari zinazotokana na matumizi ya madawa ya kulevya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles