27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Yafahamu maneno hatari kusemwa kwa mpenzi wa kike

NA DK. CHRIS MAUKI


KUFAHAMU haya maneno kutakusaidia wewe mwanaume kuongeza ubora wa mahusiano yako na mpenzi wako.

Yamkini vitu hivi ni vya kweli na halisi lakini kule kuvitamka mbele ya mpenzi wako wa kike huamsha hamaki, hasira au huzuni. Maneno haya ni kama vile;

Yule rafiki yako mzuri sana, anavutia sana, anafiga nzuri

Sentensi kama hii humpa hofu mpenzi wako kuwa yamkini unamtamani rafiki yake na matokeo yake mara zote anakuwa asiye na amani “insecured” hasa mara nyingine mnapokutana na huyo rafiki. Hata kama anakuvutia au amependeza kuliko mpenzi wako, kaa nayo moyoni au tumia busara zaidi kuiwakilisha.

Natamani upungue huo mwili, anza kupunguza chakula?

Wanawake wengi hupenda kusikia habari nzuri kuhusu miili yao, hata kama miili hiyo haiko vizuri kama wanavyodhani, habari yeyote kinyume cha hapo huwakasirisha. Usiruhusu wajue au ajue kuwa umeyatambua mapungufu  yake kimwili, kwa sababu labda tayari yeye yana muudhi. Unaweza kutumia busara kumfikishia ujumbe wa hicho hicho unachotamani kumwambia na ukakuta kinafanyika pasipo kuamsha misuguano.

Sipendi kabisa kuoa, sidhani kama nitaoa

Maneno haya huathiri zaidi wale walio katika mahusiano, tena mahusiano ya muda mrefu na mmoja wapo akitamani hasa kuona wanaingia katika ndoa, wanawake  hususani huwa na kiu ya kudumu katika mahusiano. Hakuna asiyependa harusi, unapomwonyesha kuwa hutamani ndoa na wakati unapenda kuwa kwenye mahusiano na yeye unamaanisha hakuna haja ya hayo mahusiano yenu, na moyoni mwake anajiuliza kama haupendi kabisa kuoa unafanya nini na yeye? Au ndiyo umeamua kumpotezea muda au kumtumia?

Mpenzi wangu wa awali alipenda kufanya hivi na alifanya tofauti na wewe

Kamwe hakuna mwanamke anayependa au aliyetayari kulinganishwa na mwingine, haswa anapolinganishwa na aliyewahi kuwa mpenzi wako. Hata kama ni ukweli kabisa kuwa uliwahi kuwa na mpenzi mwingine, na hilo analijua, ila sio afya kumwongelea au kumtajataja mara kwa mara unapokuwa na mpenzi wako wa sasa. Kwa kufanya hivi hautomaliza wivu kwa mpenzi wako wasasa. Mara nyingi kwa kumkumbusha au kumtajataja mara kwa mara, yeye anaweza hufikiri bado unahisia na mpenzi huyo wa zamani.

Nafikiri tusiende pamoja/Nadhani sina haja ya kwenda na wewe

Kama kuna uwezekano wa mpenzi wako kufuatana na wewe basi mpe nafasi. Kama hakuna kabisa uwezekano tafuta lugha nzuri ya kumshawishi kwamba hautoweza kwenda naye. Kukataa kwa maneno makavu kwaweza kumfanya atafsiri kwamba unafanya hivyo kwasababu binafsi au haujisikii furaha kuwa naye karibu au labda yeye anakuaibisha unapokuwa naye. Maswali haya yote na hisia hizi haziwezi kumwacha salama. Usisahau kwamba muda mwingi mnaotumia pamoja huboresha penzi lenu, na mwanamke yeyote hutamani kuwa na muda mrefu na mpenzi wake, labda kuliko hata wewe unavyotamani.

Hiyo hewa uliyotoa ni kali sana (inanuka sana), kwanini uchafue hewa kiasi hicho?

Kama mko karibu sana kimahusiano na mnaweza kuwa na utani wa viwango fulani, hii yaweza kuwa sawa kwenu, lakini kama hamko karibu sana, na yamkini ukaribu wenu haujafikia kiwango hicho, kamwe usionyeshe umegundua utofauti wa harufu au tofauti yoyote iliyotokea kwenye hali ya hewa hata kama una uhakika yeye ndiyo mhusika aliyeharibu hewa. Kamwe usimcheke kwasababu yamkini hali hii inaweza kumsumbua sana, hususani anapotambua kuwa umegundua wazi jambo hilo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles