29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

World Vision yatoa vyandarua kwa watoto Itilima kupambana na Malaria

Derick Milton, Itilima

Shirika la World Vision Tanzania kupitia mradi wake wa Kanadi katika Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu limetoa zaidi ya vyandarua 6,000 vyenye viuatilifu vinavyodumu muda mrefu kwa watoto waishio mazingira hatarishi wilayani humo.

Vyandarua hivyo vimetolewa kwa watoto wapato 6,160 kutoka katika vijiji mbalimbali Wilayani humo lengo likiwa ni kuwalinda dhidi ya ugonjwa wa Maralia ambao katika wilaya hiyo umekuwa ukiadhiri zaidi watoto.

Akiongea katika hafla ya kukabidhi vyandarua hivyo kwa watoto leo katika kijiji cha Nanga, Mratibu wa Mradi kutoka World Vision, Nyamoko George amesema kuwa utolewaji wa vyandarua hivyo ni moja ya shughuli ambazo zimekuwa zikifanywa na shirika hilo katika kuwalinda na watoto.

“ Katika kuendelea kuwalinda watoto shirika liliona ni vyema kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa Maralia ambapo, tutawapatia watoto ambao tumekuwa tunawafadhili 3,431 na wengine ambao hatuwafadhili 2,729,” amesema George.

Akitoa taarifa ya hali ya Malaria katika Wilaya hiyo, Mganga mkuu wa Wilaya Dkt. Anold Msiba amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa idadi kubwa ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanaambukizwa ugonjwa huo.

Amesema hamashuari kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wameendelea kupambana na ugonjwa huo ambao kiwango cha maambukizi wilaya ni asilimia 5.1 ya kiwango cha kitaifa.

Amesema kuwa katika mapambano hayo wamegawa vyandarua kwa mama wajawazito na watoto waliotimiza miezi tisa kupitia mpango wa Chandarua Kliniki na kugawa vyandarua 95,840 toka mwaka 2017 hadi 2020.

“ Tumegawa kwa mama wajawazito 47,517 na watoto chini ya umri wa mwaka mmoja 48,323, lakini pia tumegawa kwa wanafunzi wa shule za msingi jumla ya vyandarua 65,854 kupitia mpango wa chandarua shuleni,” amesema Msiba.

Akipokea vyandarua hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Benson Kilangi, Katibu tawala wa Wilaya hiyo, Filbert Kanyirizu aliwataka wazazi na walezi wa watoto hao kuhakikisha wanavitumia vyandarua hivyo kwa kazi iliyokusudiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles