30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TWCC yazindua tuzo za wanawake wajasiriamali

Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), kimezindua tuzo za wanawake waliofanya vizuri zaidi kwa mwaka 2020 katika sekta za viwanda na biashara zenye lengo la kutambua na kuheshimu wanawake waliofanikiwa na wale wanaochipukia katika sekta za viwanda na biashara.

Tuzo hizo zimezinduliwa leo Jumatano Septemba 9, jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa chama hicho, Jacquiline Maleko ambapo amesema kuwa tuzo hizo zinalenga kuonesha mchango wa mwanamke mjasiriamali katika kukuza uchumi wa nchi na kuchochea maendeleo ya jamii.

Akizungumza katika uzinduzi huo Jacquiline mesema wanawake ni nguzo muhimu sana katika maendeleo ya jamii yoyote na kwamba wana uwezo wa kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya viwanda na biashara endapo wataaminiwa na kupewa nafasi yakufanya hivyo.

“Tunaishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini ambapo wanawake wengi wameweza kuanzisha biashara na viwanda vidogo ambavyo vimewaongezea kipato, kuzalisha ajira pamoja kuchangia katika kukua kwa uchumi wa nchi.

“Juhudi zinazofanywa na serikali kwa sasa katika kuboresha mazingira ya biashara zinatia moyo na tunawaomba wadau wote washirikiane na serikali hasa katika kutekeleza mpango wa uboreshaji wa mazingira ya biashara yaani ‘The Blueprint for Regulatory Reforms to Improve the Business Environment’.

“Mchakato wa upatikanaji wa washindi wa tuzo unaratibiwa na kamati maalum inayoundwa na wajumbe kutoka taasisi za serikali na sekta binafsi, ili kuweza kushiriki katika tuzo hizi wanawake wanatakiwa kujaza fomu maalumu ambazo kwa sasa zinapatikana bure katika tovuti ya TWCC www.twcc-tz.org, Ofisi za serikali za mikoa, Halmashauri, ofisi za TWCC Mikoa mbalimbali, SIDO na ofisi zote za TCCIA,” amesema Jacquiline.

Jacquiline ameongeza kuwa zoezi la kusajili washiriki wa tuzo litaendelea kwa kipindi cha mwezi mmoja na litafungwa Oktoba 9 mwaka huu na kwamba sherehe za utoaji wa tuzo kwa washindi zinatarajiwa kufanyika Novemba 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Amesema utoaji wa tuzo hizo utaambatana na uzinduzi wa Jarida la Wanawake 100 Wajasiriamali waliothubutu kitachotumika kutangaza kazi mbalimbali za wanawake wajasiriamali nchini.

“Tuzo za mwaka huu zinafadhiliwa na TradeMark East Africa (TMEA) chini ya mradi wa kujengea wanawake uwezo wa kufanya biashara na wamekuwa wakifadhili TWCC toka mwaka 2016 kujenga uwezo wa wanawake kuuza bidhaa ndani ya Jumuiya ya Afrika mashariki.

“Kupitia mradi huu TMEA imeshafikia zaidi ya wanawake 3000 na ina mpango wa kufikia jumla ya wanawake 10,000 kupitia TWCC ifikapo mwaka 2023, TMEA imetenga zaidi ya shillingi bilioni mbili kufanikisha mradi huu wa kujengea uwezo wanawake wa Tanzania kufanya biashara,” amesema Jacquiline.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles