29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

WMA yatoa wasiwasi wananchi

Na Mwandishi Wetu, Simiyu

WAKALA wa Vipimo (WMA), imewataka wananchi kutokuwa waoga wa kutoa taarifa zitakazowafichua wale wote wanaojihusisha na kuchezea na kuharibu nipimo kwa lengo la kuwapunjawauzaji wa bidhaa mbalimbali.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa Wakala, Deogratius Maneno katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu, wakati wa maonesho ya Nanenane yanayoendelea.

Alisema taarifa zitolewe kupitia ofisi zao zilizopo mikoa yote ya Tanzania Bara au kupitia namba yao ya simu ya  bure ambayo ni 0800 11 00 97 ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Maneno aliwataka wafanyabiashara kufanya kazi zao kwa uadilifu na kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa kwani adhabu zitolewazo kwa wakiukaji wa Sheria ya vipimo ni kali.

Kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Vipimo Sura na. 340 na mapitio yake, endapo mtu yeyote atabainika kutenda kosa kinyume na sheria hiyo na akakiri kutenda kosa husika, atapaswa kulipa faini isiyopungua Sh 100,000 na isiyozidi Sh milioni 20,000,000 kwa kosa la kwanza.

Alisema endapo mtuhumiwa atakataa kukiri kosa na kufikishwa mahakamani kwa kosa hilo na akabainika kutenda, atatozwa faini isiyopungua Sh 300,000 na isiyozidi Sh 50,000,000 au kifungo kisichozidi miaka miwili au vyote kwa pamoja.

 Alisema endapo mtuhumiwa atakamatwa na kosa kwa mara ya pili na kuendelea na akipelekwa mahakamani akakutwa na hatia, adhabu ni faini isiyopungua Sh 500,000 na isiyozidi Sh milioni 100 au kifungo kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja.

Alisema kazi hiyo,imelenga kuhakikisha kunakuwa na biashara ya haki kati ya mteja na mamlaka za maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles