23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kutumia kondomu zilizopitwa wakati zina madhara makubwa

Na AVELINE  KITOMARY-DAR ES SALAAM

KAIMU Mkurugenzi wa Dawa na Vifaa Tiba  wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba(TMDA), Akida Khea amesema yapo madhara makubwa kiafya endapo mtu atatumia kondomu ambazo hazijathibishwa usalama  na ubora wake.

Akizungumza na wakati wa mahojiano maalumu  MTANZANIA, Dar es Salaam jana,  Khae alithibitisha madhara yanayotokana na matumizi ya kondom zisizo  na ubora ni kuambukizwa virusi vya Ukimwi pamoja na magonjwa ya zinaa.

Kutokana na hilo, Khea alisema ni bora watumiaji kuhakikisha ubora wa kondom wanazozitumia  ili kuepusha madhara hayo.

“TMDA kwa sasa imebki na jukumu la kulinda afya ya jamii  kwa kudhibiti  ubora,usalama  na ufanisi wa dawa ,vifaa tiba na vitendanishi,bidhaa kama kondomu isipokubalika tunasema haina ubora kwa matumizi  nchini.

“Kama kondomu  ikithibitishwa haina ubora,ikitumika haiweza kumlinda mtumiaji  kwa magonjwa  ya kujamiana na Ukimwi… kondomu kama hizi ni hatari kwa afya.

“Huwa tukigundua hazina ubora  tunaziondoa haraka kwenye soko, ni vizuri jamii wakatumia zilizothibitishwa, pia ni vizuri wakatoa  taarifa endapo watakutana na kondomu zisizo na ubora,”alieleza Khea.

Alitoa wito kwa jamii kuaangali mwisho wa matumizi ya bidhaa (expire date), hasa  kwa bidhaa kama kondomu ili kulinda afya zao wenyewe.

“Kama una bidhaa ambazo huna uhakikia nazo ni vizuri ukatoa taarifa TMDA ili tukafanyie uchunguzi na tubaini usalama na ubora wake,”alisshauri Khea.

Katika mwaka wa fedha 2019/20,  TMDA ilifakiwa kuondoa sokoni pakiti 17,076, baada ya kushindwa kukidhi vigezo vinavyotakiwa.

Kondomu hizo zilizoondolewa sokoni ni aina tano ambazo ni Life Guard, Ulitimate, Maximum Classic,Prudence naa Chishango.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles