29.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

Makonda ampa neno mrithi wake

A BRIGHITER MASAKI-DAR ES SALAAM

ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkuu wa Mkoa mpya, Aboubakar Kunenge.

Alisema ataendelea kusimama kidete kumlinda na kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli kwa kila jambo kwa kuwa ndiyo “role model”wake. 

Akizungumza na waandishi wa habari, baada ya makabidhiano hayo Ilala,Dar es Salaam jana, Makonda alisema anajisikia amani na furaha  kumaliza safari yake ya utumishi ndani ya mkoa akiwa ameacha alama kubwa kwa jamii, taasisi na kugusa maisha ya mtu mmoja mmoja.

“Nitaendelea kuwa mshauri wa mambo mbalimbali yenye kuleta maendeleo kwa mkoa na taifa kwa ujumla kwa kuwa yapo mengi niliyojifunza katika safari yake ya utumishi,”alisema.

Alisema kwa sasa analo jukumu la kuendelea kuhakikisha Rais Magufuli anapata ushindi wa kishindo wakati wa uchaguzi mkuu, ikiwa ni pamoja na kupata wabunge na madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Hakuna mamlaka yanayotoka nje ya Mungu, nimeitumikia kwa muda wa ukamilifu wa miaka mitano, miezi mitatu na siku nne kwa kuitii sauti ya Mungu, Rais aliniamini na kunichagua katika wengi wasioniamini na kuweka imani yake kwangu,”alisema.

Alisema  ana taarifa nyingi maelezo mengi Magufuli aliamini katika vijana na kumchagua kuwa  wa kwanza kupewa majukumu kuutumikia mkoa mkubwa na kuacha alama itakayokumbukwa milele yote.

“Baada ya kuteuliwa nikaanza kazi namshukuru kwa mengi ikiwemo uvumilivu wake alionivumilia pindi mbwa mwitu walipokuwa wakibweka,Rais Magufuli akaendelea kuniamini hatimaye tarehe 15 nimeondoka mwenyewe ikiwa ni ishara ya kukubali kazi nilioifanya na na kuamini kuendelea na majukumu mengine.

“Nimepita katika changamoto kubwa na  vita nyingi,kubwa ni moja  ya madawa ya kulevya ambayo kila mtu alinipigia kelele na kunipinga,Dk. John Magufuli hakuwahi kuyumba misimamo yake alibaki kuniamini na kuamini ninachokifanya ni kwa maslahi ya wananchi hatimaye mkoa tukaibuka kidedea kupiga vita dawa za kulevya,”alisema.

“Nilimwambia ukiona unapingwa vita hujuwe wewe unakitu kikibwa na chatofauti na wao ndio sababu ya kuzungumziwa mitandaoni,” alisema. 

Alimuomba Kunenge kukamiliaha kumkabidhi barabara Askofu Kardinali Pengo iliyopewa heshima ya jina lake, pamoja na barabara ya mchezaji wa kimataifa Mbwana Samata kwa heshima aliyoipatia taifa la Tanzania kimataifa kupitia michezo. 

“Nawapenda wananchi wa Dar es Salaam, namewatumikia vema kwa kutumia akili na vipaji vyangu vyote na endapo nilikwenda kinyume na matakwa yenu naomba mnisamehe niwaombe mkisikia nimemuacha Yesu ndio muuzunike lakini kama Yesu ninae nina amani moyoni na furaha ya kutosha”alisema Makonda

Alimuomba Kunenge awaache bodaboda waendelee kutumia jiji lao kujipatia kipato chao cha kila siku. 

Kunenge alisema ataendelea kupokea ushauri mbalimbali anaopatiwa na Makonda kwakuwa amekuwa mwalimu na mshauri wake katika mambo mbalimbali tokea walipoanza kufanya kazi pamoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,701FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles