20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara yadai kodi ya ardhi mlango kwa mlango

NYUMBA KWA NYUMBA: Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akizunguma na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa, wakati alipokwenda ofisi za shirika hilo kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni maofisa kutoka wizara hiyo pamoja na shirika la reli.PICHA: WIZARA

Na Munir Shemweta

NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula, ameanza operesheni ya kuzibana taasisi ambazo ni wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika jiji la Dara es Salaam kwa kutembelea ofisi moja hadi nyingine ili zilipe madeni yao katika muda uliopangwa.

Katika ziara hiyo taasisi sita kati ya saba alizotembelea ziliahidi kulipa zaidi ya Sh bilioni 4.5 kufikia Desemba 19.

Taasisi alizotembelea ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linalodaiwa Sh bilioni 3, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Sh bilioni 1.4, EPZA milioni 200, Shirika la Reli Tanzania (TRC) Sh bilioni 2.5, Shirika la Masoko Kariakoo milioni 249 na Chuo cha Taifa cha Utalii milioni 26.8.

Akiwa katika Shirika la Masoko Kariakoo, Dkt Mabula alishangazwa na shirika hilo kudaiwa zaidi ya milioni 200 huku likiomba kulipa deni lake katika kipindi cha miaka miwili jambo alilosema ni kinyume na taratibu za ulipajia madeni ya kodi ya pango la ardhi ambazo humtaka mdaiwa kulipa nusu ya deni.

Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariako, Hetson Kipsi, katika barua yake, Shirika lake liliahidi kulipa kwa awamu deni hilo katika kipindi cha miaka miwili kwa kutoa milioni saba kila mwezi jambo lililokataliwa na Dkt Mabula.

Alisema shirika hilo linapaswa kulipa nusu ya deni kwanza ndipo liingie makubaliano ya kulipa kiasi kilichobaki kwa awamu.

Kwa upande wa TRC,  Mkurugenzi Mtendaji wake Masanja Kadogosa,  Dk Mabula kuwa shirika lake halipingi kulipa deni inalodaiwa bali linachofanya ni kulihakiki upya deni hilo kwa kuwa kumekuwa na uhamisho wa umiliki wa mali za TRC kwenda TBA tangu mwaka 1999 sambamba na baadhi ya nyumba za Shirika kuuzwa kwa wananchi huku baadhi ya mali za TRC zikiwa hazina hati.

Kadogosa alisema, kiasi cha Sh bilioni 2.4 wazodaiwa ni kikubwa na hakilingani na uhalisia wa deni la TRC na kubainisha kuwa uhakiki utakapokamilika ana imani deni hilo litapungua kwa kiasi kikubwa.

 Dkt Mabula alimueleza kuwa Kadogosa, shirika lake linapaswa kulipa robo ya tatu ya deni hilo wakati uhakiki ukiendelea na iwapo itaonekana deni limepungua basi kiasi cha fedha kilichozidi kitarudishwa. 

Kadogosa alikubali kulipa Sh milioni 400 kwa awamu hadi kufikia oktoba 2019 wakati zoezi la uhakiki wa deni hilo unaohusisha Wataalamu wa Shirika hilo na Wizara ukiendelea.

Chuo cha Taifa cha Utalii kupitia kwa Kaimu Mkuu wa Chuo, Boniface Mwaipaja, kilikiri kudaiwa milioni 26.8 na kuahidi kulipa kwa awamu deni hilo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles