25.4 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Mifugo na Uvuvi yataja mafanikio miaka 60 ya Uhuru

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imetaja mafanikio ambayo imeyapata katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, huku ikidai  itahakikisha kuwa sekta ya mifugo inaendeshwa kibiashara ili kuleta tija kwa wafugaji na Taifa kwa ujumla.

Pia itahakikisha kuwa rasilimali za uvuvi zinasimamiwa ipasavyo ili kuwa na uvuvi na ukuzaji viumbe maji endelevu, maendeleo ya viwanda, ukuaji wa kipato cha mtu mmoja mmoja na pato la Taifa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Alhamisi  Novemba 25,2021,Waziri wa Wizara hiyo,Mashimba Ndaki, wakati akitaja mafanikio ya wizara hiyo amesema sekta ya uvuvi ni miongoni mwa sekta za uzalishaji mali ambayo ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na miongozo ya usimamizi na uratibu wa uendeshaji wa shughuli za uvuvi nchini.

“Katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara Wizara yangu   itahakikisha kuwa sekta ya mifugo inaendeshwa kibiashara ili kuleta tija kwa wafugaji na Taifa kwa ujumla,”amesema.

Aidha amesema wizara itashirikiana na wadau mbalimbali wa sekta binafsi ili kukuza na kuendeleza sekta za mifugo na uvuvi kwa kasi zaidi, chini ya uongozi mahiri wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Ulaji, ubora wa nyama Tanzania

Kuhusu ulaji wa nyama nchini, Waziri huyo amesema Watanzania wamekuwa na changamoto ya kula nyama na kunywa maziwa ambapo amedai kwa mwaka mtu mmoja anatakiwa kula nyuma kilo 50 na maziwa lita 200.

Amefafanua kuwa  kiwango cha ulaji wa samaki kwa sasa ni kilo 8.5 kwa mtu  mmoja kwa mwaka ikilinganishwa na kiwango kinachopendekezwa na Shirika na Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) cha kilo 20.3 kwa mwaka.

Ndaki amesema nyama ya Tanzania ina ubora na ndio maana  imekuwa ikinunuliwa na Nchi nyingi kutokana na ubora huo huku akiztaja nchi ambazo zimekuwa zikinunua nyama ya Tanzania kuwa ni Oman,Kuwait,Qatar,Vietnam.

Katika hatua nyingine, amesema Serikali imetenga maeneo ya malisho ya wafugaji hasa katika kipindi cha kiangazi lengo likiwa ni kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji.

Ulinzi kuimarishwa rasilimali za uvuvi

Amesema Tanzania ilianza juhudi za kulinda na kudhibiti rasilimali za uvuvi tangu ilipotunga sheria ya kwanza ya uvuvi iliyoitwa ‘Fisheries Ordinance and Trout Protection Ordinance CAP 368’.

Amesema tangu nchi yetu ipate Uhuru, juhudi mbalimbali zimefanyika ili kuwezesha usimamizi endelevu wa rasilimali za uvuvi zikiwamo kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali, kuanzisha Kanda nne (4) na vituo 35 vya doria.

Bilioni 50 ujenzi bandari ya uvuvi Kilwa Masoko

Waziri huyo amesema wizara inaendelea kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ya Uvuvi kupitia mtaalam mwelekezi ambaye ni Kampuni ya M/S Sering Ingegneria ya nchini Italia kwa gharama ya shilingi 1,421,041,703.

Amesema Serikali tayari imechagua eneo la Kilwa Masoko kwa ajili ya kujenga bandari ya uvuvi.

Amesema katika mwaka huu wa fedha 2021/2022, Serikali imetenga kiasi cha sh 50 bilioni kwa ujenzi wa Bandari hiyo mara baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu.

Aidha, jitahada za kutafuta wawekezaji wa kujenga miundombinu mingine ya uvuvi katika eneo hilo zinaendelea vizuri.

Ataja changamoto za uvuvi

Amesema Wizara ya imefanya tathmini ya mahitaji ya samaki nchini ambapo makadirio ni tani 750,000 kwa mwaka ikilinganishwa na uzalishaji wa tani 496,390, sawa na upungufu wa tani 253,615.

Juhudi zinazoendelea za kuongeza uzalishaji wa samaki nchini zitaongeza ulaji wa samaki kwa Watanzania kufikia kilo 10.5

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles