23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATANGAZA ADA MPYA

Na Hamza Temba -Dar es Salaam

WIZARA ya Maliasili na Utalii imetangaza viwango vipya vya malipo ya ada kwa mawakala wa kusafirisha watalii nchini baada ya kukamilika kwa marekebisho ya kanuni ya ada na tozo za biashara ya utalii yaliyofanyika Desemba mwaka jana.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, imeeleza kuwa baada ya kukamilika kwa marekebisho ya kanuni, tangazo la Serikali namba 506 la Desemba 29, mwaka jana limeweka viwango vipya vya ada kwa mawakala wa kusafirisha watalii.

Alivitaja viwango hivyo kuwa ni Shilingi 1,112,500 sawa na Dola za Marekani 500 kwa kampuni za wazawa zenye umiliki mkubwa wa raia wa Tanzania na zinazomiliki gari 1 hadi 3.

“Shilingi sawa na Dola za Marekani 2,000 kwa kampuni zenye gari 4 hadi 10, shilingi sawa na Dola za Kimarekani 3,000 kwa kampuni zenye gari 11 hadi 50 na shilingi sawa na Sola za Kimarekani 5,000 kwa kampuni zenye kumiliki gari 51 na kuendelea,” alisema Milanzi katika taarifa hiyo.

Alisema kwa upande wa kampuni za kigeni zenye umiliki mkubwa wa raia wa kigeni na zinazomiliki gari 10 hadi 30, zitalipa ada ya shilingi sawa na Dola za Marekani 5,000, kampuni zenye gari 31 hadi 50 zitalipa shilingi sawa na Dola za Marekani 7,500 na kampuni zenye gari 51 na kuendelea zitalipa shilingi sawa na Dola  za Marekani 10,000.

Kutokana na marekebisho hayo, muda wa kutumika kwa leseni za mwaka 2017 za wakala wa kusafirisha watalii  umesogezwa mbele hadi Januari 31,  mwaka huu  ili kuwezesha maandalizi ya kuingia kwenye mabadiliko ya viwango hivyo vipya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles