23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Kilimo kudhibitisha udhaifu miradi ya umwagiliaji

Ramadhan Hassan-Dodoma

Wizara ya Kilimo imesema imeona udhaifu mkubwa katika miradi ya umwagiliaji hivyo imeunda timu maalum kulishughulikia hilo.

Hayo yameelezwa  leo Jumatatu Mei 20 Bungeni na Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba  wakati ahitimisha  mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, kwa mwaka wa fedha 2018-2019.

Mgumba amesema ripoti ya CAG imeonesha kuna udhaifu mkubwa katika miradi ya umwagiliaji nchini hivyo Wizara ya Kilimo imeunda timu maalum kwenda kudhibitisha hayo.

“Ili wote wachukuliwe hatua na tujifunze wapi tulipofanya vibaya tutaunda mapitio ya kimuundo badala ya Tume ya Umwagiliaji kuwa katika Kanda tutaipeleka mpaka katika kata na vijiji,”amesema Mgumba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles