25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Shabiki wa Real Madrid ashinda milioni 208.5 za M-Bet

Mwandishi wetu-Dar es Salaam

Mkazi wa Ifakara, mkoani Morogoro, Gadi Mwajeka (37) ambaye pia shabiki wa timu ya Real Madrid ameshinda kiasi cha Sh 208, 574, 790 baada ya kubashiri kwa usahihi mchezo wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi,  Mwajeka  amesema kuwa hakuamini mara baada ya kupigiwa simu kuambiwa kushinda kiasi kikubwa cha fedha.

Mwajeka ambaye ni mfanya biashara ya rangi za mkeka Ifakara mjini amesema kuwa ushindi huo ni faraja kubwa sana kwake kwani utamwezesha kuipanua biashara yake na kuanzisha nyingine.

“Sikuamini kama nimeshinda kiasi kikubwa cha fedha, nimetumia kiasi cha sh1,000 tu kubashiriki na kuingia kiasi kikubwa cha fedha. Nimefarijika sana,” amesema Mwajeka.

 “Mke wangu ni nesi, nilikuwa nachukua madaftari yake kuandika timu na kuanza kuzipigia mahesabu, nitatumia fedha hizi kwa ushauri wa wazazi wangu kuona ninafanya biashara gani,” amesema.

Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi Mushi amesema kuwa  M-Bet itaendelea kuwa nyumba ya mabingwa na kuwaomba mashabiki wa soka kubashiri na kampuni yao ili kuweza kubadili maisha.

“M-Bet ni nyumba za mabingwa na mabingwa wote wanapatikana kupitia michezo ya kubahatisha ya kampuni yetu na kujitajirisha vile vile vile kuichangia nchi yao kwani asilimia 20 ya fedha hukatwa kama kodi ya kusaidia maendeleo ya nchi katika sekta mbalimbali,” amesema Mushi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles