25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wito watolewa kutenga bajeti kuhudumia watoto waliopoteza malezi

Tunu Nassor-Dar es Salaam

Shirika linalojishughulisha na watoto waliopoteza au walio hatarini kupoteza malezi la SOS, limeziomba halmashauri nchini kutenga bajeti ya kutosha kuhudumia malezi ya watoto hao ili kupunguza changamoto kwa maofisa wanaohudumia.

Akizungumza katika semina ya kuwajengea uwezo maofisa ustawi wa jamii wa jiji la Dar es Salaam, Mratibu wa Mpango wa Malezi Mbadala katika jamii kutoka SOS, Husna Selungwi amesema kwa sasa bajeti ni ndogo haitoshelezi kukabiliana na changamoto hiyo.

Amesema ni vyema maofisa ustawi wa jamii kuingia katika vikao mbalimbali vya manispaa ikiwamo baraza la madiwani na takwimu kushawishi kutenga fungu la kutosha hasa watakapoona hali ilivyo.

“Kuna uhitaji wa maofisa ustawi kuingia katika vikao na kuwaambia ukweli kuwa hata watoto wao wanaweza kuangukia kwa mtu wa kuaminika hivyo ni vema kutenga fungu la kutosha kuwasaidia,” amesema Husna.

Naye Ofisa Ustawi wa Ofisi ya Mkoa huo, Flora Masue amewaomba wadau kushirikiana na serikali kuhakikisha elimu ya malezi ya mtoto inatolewa katika taasisi za elimu ili kuandaa wazazi wenye uelewa wa malezi.

“Niwaombe wadau kujitokeza kusambaza elimu ya malezi katika vyuo ili wanapojiandaa kuwa wazazi wajue namna ya kulea,” amesema Flora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles