Addis Ababa, Ethiopia
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema bara la Afrika linatakiwa kupata chano zaidi kutokana na wimbi la tatu la maaambukizi ya Ugonjwa wa Covid 19.
Ripoti hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa WHO wa kanda Afrika, Matshidiso Moeti alisema idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona imepita milioni tano huku nchi saba zikiishiwa na chanjo.
Pia ameongezea na kusema Afrika inahitaji mamilioni zaidi ya chanjo kwa sasa.
Afrika Kusini, Morocco, Tunisia, Ethiopia na Misri zimerekodi viwango vya juu zaidi vya maambukizi ya Corona barani humo.
Uganda na Namibia zinakabiliwa na wimbi la tatu la maaambukizi huku makumi ya watu wakiripotiwa kufa kila siku.
Jumla ya watu elfu136,030 wamefariki kutokana na ugonjwa wa Covid -19 katika nchi tofauti za Afrika, kulingana na takwimu zinazotolewa na shirika la Afya Duniani WHO.
Kirusi cha Delta kimegunduliwa katika nchi 14 za Afrika huku kirusi cha Beta, kilichogunduliwa mara ya kwanza Afrika Kusini , kikifika katika nchi 25.
WHO inasema hakuna muda kamili ulitowa kubaini ni lini chanjo zaidi zitapatikana lakini limesistiza kwamba kuna haja kushughulikia upatikanaji wake kwa dharura.