26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Iran yafanya uchaguzi wa Rais

Debeni, Iran

Nchi ya Iran imefanya Uchaguzi mkuu wa kumchagua Rais wa kuliongoza Taifa hilo huku mmoja wa mgombea wa kiti hicho anatarajiwa kumrithi Hassan Rouhani.

Kiongozi wa kidini wa Shia , Ebrahim Raisi ambaye ni mhafidhina anayeongoza mahakama, ndiye anayependelewa kuchukua wadhifa wa uongozi wa Taifa hilo kulingana na kura za maoni.

Wapinzani na baadhi ya wanaopendelea mabadiliko wametoa wito wa kususiwa kwa uchaguzi, wakisema kuzuiwa kwa wagombea kadhaa kushiriki uchaguzi huo kumefanya Raisi kutokuwa na upinzani wa kisawa sawa.

Kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Ali Khamenei amepiga kura yake mapema Ijumaa katika mji wa Tehran na kuhamasisha raia kujitokeza kupiga kura.

Kuna minung’uniko mingi miongoni mwa raia wa Iran kuhusiana na changamoto za kiuchumi ambazo wamekumbana nazo tangu Marekani ilipojiondoa katika mpango wa nyuklia wa Iran miaka mitatu iliyopita na kuwekewa tena vikwazo vilivyolemaza nchi hiyo.

Ushindi kwa mmoja wa wenye msimamo mkali hakutarajiwi kutatiza mazungumzo kati ya Iran na nchi zenye nguvu duniani ambayo lengo ni kuyafufua tena, kulikofanya Iran kukubali kupunguza kasi ya mpango wake wa nyuklia katika sehemu ya mabadilishano ya kuondolewa kwa vikwazo.

Takriban wagombea 600 wakiwemo wanawake 40, walishiriki zoezi la kutaka kuingia debeni.

Lakini mwisho wa siku ni wanaume saba pekee ndio walioidhinishwa mwezi jana na mahakimu 12 na wanatheolojia wa Baraza la Guardian, bodi yenye kufanya maamuzi kuhusiana na wagombea waliotimiza vigezo vya kugombea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles