26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wilshere: Klabu hazinitaki, acha nistaafu

London, Uingereza

KIUNGO wa zamani wa Arsenal, Jack Wilshere, amesema anafikiria kuachana na soka kwa kuwa hakuna klabu iliyomfuata kutaka kumsajili.

Wilshere (29), amekuwa mchezaji huru tangu alipotemwa na Bournemouth, klabu ya Ligi Daraja la Kwanza England (Championship) aliyoitumikia kwa miezi sita tu.

Akizungumzia hatua yake ya kutaka kustaafu, Wilshere aliyewahi kutamba na timu ya taifa ya England, anasema: “Kama ningekuwa kwenye kiwango kizuri, klabu zingekuja na kunipa nafasi…”

Nyota huyo aliibuliwa na ‘academy’ ya Arsenal na kisha kuitumikia timu ya wakubwa kwenye michezo 197, kabla ya kutimkia West Ham United mwaka 2018.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles