27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Will Simth: Kujiamini, kujituma, nidhamu ni urithi kutoka kwa baba

will-smith

Na BADI MCHOMOLO

NI siku tano sasa tangu nguli wa filamu na muziki nchini Marekani, Will Smith, apate majonzi kutokana na kumpoteza baba yake mzazi Willard Carroll Smith Sr.

Imekuwa ni wiki ya majonzi kwa familia ya Smith, kutokana na marehemu kuacha maneno mazito wakati wa uhai wake kwenda kwa watoto wake pamoja na wajukuu.

Smith Sr, alikuwa mpambanaji katika maisha yake japokuwa hakufanikiwa sana kama ilivyo kwa mtoto wake Will Smith ambaye ana jina kubwa katika tasnia ya filamu na muziki.

Will Smith baada ya kifo cha baba yake ameweka wazi jinsi alivyolelewa na baba yake hadi anafanikiwa huku baba yake akiwa hana jina kubwa kama alivyo yeye.

“Baba yangu hakuwa na jina kubwa sana duniani kama nilivyo mimi, lakini aliweza kupambana kwa ajili ya watoto wake waweze kuwa na majina makubwa na utajiri.

“Kwa hatua hiyo alifanikiwa, lakini katika familia kuna maneno ambayo hatuwezi kuyasahau ambayo alikuwa anayaongea kwa ajili ya sisi kuweza kupigania maisha, aliwahi kusema, ‘Kama umekamilika kiakili, mwili, ni vizuri kupambana na maisha.

‘Maisha yapo vilevile, lakini kikubwa kinachotakiwa ili  ufanikiwe ni kupambana, kujiamini, kujitambua na kujituma, ipo siku nitaondoka duniani na muyaweke wazi maneno yangu hasa kwa familia yangu pamoja na wajukuu kwa ujumla.

‘Hakuna njia nyingine ya kuweza kufanikiwa kama utashindwa kuyafanya hayo, naamini kila mmoja akiweza kufanya hivyo ataishi kutokana na ndoto zake.’

“Ni maneno nisiyoyasahau kamwe kutoka kwa baba yangu,” anasema Will akimnukuu baba yake marehemu mzee Smith Sr.

Will Smith ameweka wazi kuwa alikuwa anayatumia maneno hayo ambayo yalisemwa na baba yake na ndiyo maana amefanikiwa na anazidi kufanya vizuri katika mambo mbalimbali ikiwa pamoja na kazi zake za muziki na filamu.

“Kila siku baba yangu alikuwa ananiambia maneno hayo wakati nakua, niliweza kuyaweka kichwani na kuyafanyia kazi na ndiyo maana kwa sasa nipo hapa, nitaendelea kuyakumbuka maneno hayo kwa kuwa yamenifanya niwe hivi.

“Maneno hayo yapo wazi hata kwa familia ya watoto wangu, nimewaambia vile ambavyo alikuwa ananiambia baba, hivyo na wao wanatakiwa kuwa na mafanikio makubwa ikiwezekana yawe zaidi yangu,” anasema Will Smith.

Ni wazi kwamba watoto wa Smith, ambao ni Jaden na Willow, wameonekana kuwa na mafanikio makubwa  wakiwa na umri mdogo.

Jaden kwa sasa anafanya muziki na filamu, aliweza kuwateka watu katika filamu ya baba yake inayojulikana kwa jina la The Pursuit of Happyness, huku Jaden akiwa na umri wa miaka 10, kabla ya kuachia filamu yake ambayo inajulikana kwa jina la Karate Kids aliyoiachia mwaka 2010.

Kutokana na kujituma kwake, msanii huyo mwenye umri wa miaka 18, kwa sasa ana albamu mbili ambazo ni The Cool Cafe na This Is The Album.

Kwa upande mwingine mtoto wa Smith ambaye ni wa kike mwenye umri wa miaka 16, Willow, amekuwa na mafanikio kutokana na kujitambua kwake, kupamba, kujituma na nidhamu, kwa sasa ni msanii wa muziki, filamu na mwanamitindo.

Jaden na Willow, kupitia mitandao ya kijamii wamedai kuwa mafanikio waliyonayo ni kutokana na maneno ya babu yao ambayo aliyaacha kwa baba yao na sasa wanayafanyia kazi kama baba yao alivyofanya na kwamba  wataendelea kumkumbuka babu yao daima milele kwa kuwa huo ndiyo urithi walioachiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles