25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wilaya ya Maswa yatumia Bilioni 27.5 kwa miradi ya maendeleo

Na Samwel Mwanga, Maswa

Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imetumia Sh bilioni 27.5 kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwezi Machi 2021 hadi Machi mwaka huu.

Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge ameeleza hayo Alhamisi Machi 24, ofisini kwake mjini Maswa wakati akitoa taarifa ya mafanikio kwa kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu.

Amesema kwa kipindi hicho wameweza kupokea kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali katika sekta ya Elimu, Maji, Afya, Barabara, Kilimo, Mifugo, Kilimo na Maliasili.

Amesema kwa kipindi hicho wamepokea fedha nyingi ukilinganisha na kipindi kingine na hivyo kuwawezesha kukamilisha baadhi ya miradi huku mingine ikiwa kwenye hatua ya mwisho ya utekelezaji.

“Tumekuwa tukipokea fedha kutoka serikalini katika kutekeleza miradi mbalimbali katika wilaya yetu ya Maswa ila kwa kipindi hiki cha mwaka mmoja Rais Samia Suluhu aingie madarakani kwa kweli fedha zinakuja kwa wingi sana huku wilayan,” amesema.

Dc Kaminyoge amesema kwa sekta ya elimu msingi katika kipindi hicho walipokea Sh bilioni 4.1, huku elimu sekondari Sh bilioni 5.1, afya Sh bilioni 1.9 na Wakala wa barabara za mjini na vijijini(TARURA) Sh bilioni 4.3.

Ameendelea kueleza kuwa katika Sekta ya Maji ambapo Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Maswa (MAUWASA) walipokea Sh vbilioni Sh bilioni 1.7,Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) walipokea Sh bilioni 2 na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kupitia mpango wa kunusuru Kaya Masikini ukipokea Sh milioni 996.8.

Amesema katika sekta ya Maendeleo ya Jamii, makundi maalum ya Vijana, Wanawake na watu wenye uemavu kwa pamoja walipatiwa mikopo yenye thamani ya Sh milioni 254.5 kupitia vikundi vyao vilivyosajiriwa na serikali.

Dc Kaminyoge amesema kuwa katika sekta ya kilimo kiasi cha Sh bilioni 1.8 zimetumika kwa ajili ya pembejeo za kilimo cha zao la pamba ambalo ndilo zao la biashara katika wilaya hiyo  huku sekta ya Mifugo ikitumia Sh milioni 499.

Pia ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwapatia fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali na kuwaomba watendaji wote wa serikali katika wilaya hiyo kuisimamia miradi ambayo bado haijakamilka ili iweze kukamilika na kutumika kwa wananchi.

Aidha, amewaomba wananchi kuilinda na kuitunza miradi yote ya maendeleo iliyojengwa kwenye maeneo yao kwa lengo la kuwanufaisha wao na vizazi vijavyo.

“Nitoe wito kwa wananchi wa wilaya ya Maswa kuilinda na kuitunza hii miradi yote ambayo imegharamiwa na serikali kwa manufaa yetu ili iweze kutunufaisha sisi na vizazi vijavyo,” amesema Kaminyonge.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles