London, Uingereza
Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger, ni miongoni mwa wadau watakaoungana na kampuni ya Spotify kuinunua klabu hiyo.
Taarifa zimedai Wenger atashirikiana na wachezaji watatu wa zamani wa klabu hiyo ili kumpa nguvu mmiliki wa Spotify, Daniel Ek. CHANZO: BeIN Sports
Lingard kulazimisha kuondoka
KIUNGO wa Manchester United, Jesse Lingard, anatarajia kulazimisha kuondoka zake Old Trafford mwishoni mwa msimu huu.
Lingard anayecheza kwa mkopo West Ham, haoni sababu ya kurudi Man United kwa sababu hana uhakika wa namba chini ya Ole Gunnar Solskjaer. CHANZO: Eurosport
Chelsea wammezea mate Pedraza
KLABU ya Chelsea inavutiwa na mpango wa kumsajili mlinzi wa pembeni wa Villarreal, Alfonso Pedraza.
Endapo watamkosa, Blues watahamishia ‘majeshi’ kwa beki mwingine anayecheza Atalanta ya Italia, Robin Gosens.
CHANZO: Caught Offside
Kigogo afunga mjadala wa Messi
RAIS wa zamani wa Barcelona, Jordi Mestre, amesema hakuna uwezekano wa Lionel Messi kuondoka klabuni hapo.
Messi mwenye umri wa miaka 33, ataongeza mkataba mpya licha ya kutakiwa PSG na Manchester City, kwa mujibu wa Mestre. CHANZO: Talksport
Arsenal chalii kwa Odegaard
REAL Madrid hawamuuzi kiungo wao raia wa Norway anayecheza kwa mkopo Arsenal, Martin Odegaard.
Hilo ni pigo kwa Washika Bunduki kwani wamekuwa wakipanga kumsajili moja kwa moja mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. CHANZO: AS
Salah akisepa, Sancho anaingia
LIVERPOOL watamgeukia winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho, endapo watampoteza staa wao, Mohamed Salah.
Salah amekuwa akihusishwa na Barcelona na Real Madrid, hivyo kocha Jurgen Klopp anaona itakuwa ngumu kumbakiza nyota huyo raia wa Misri.
Hata hivyo, changamoto inayoweza kuikumba Liverpool ni dau la Pauni milioni 120 linalotakiwa na mabosi wa Dortmund.
Bellingham mshahara mara mbili Dortmund
ILI kumshawishi asiondoke Borussia Dortmund, klabu hiyo imepanga kuongezea mara mbili ya mshahara wanaompa staa wao, Jude Bellingham.
Hiyo ni katika juhudi zao za kumzuia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 asiende Chelsea.
Bellingham amekuwa mchezaji muhimu wa Dortmund tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Birmingham City mwaka jana.
Tottenham kubeba wawili Tottenham
MABOSI wa Tottenham wanajipanga kumsajili beki wa kati wa Fulham, Joachim Andersen, sambamba na kiungo wa Celtic, Ismaila Soro.
Hata hivyo, Tottenham watakabiliana na Manchester United na Chelsea ambazo pia zinamtolea macho Andersen.
Soro, licha ya kwamba amecheza mechi 20 msimu huu, ameingia kikosi cha kwanza cha Celtic mara moja tu tangu Februari, mwaka huu.