23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Waandishi wa Habari Mwanza wajengewa Uwezo wa Kisheria

Clara Matimo na Sheila Katikula,Mwanza

Wakati Tanzania inatarajia kuungana na nchi zingine duniani kuadhimisha siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani inayoadhimishwa Mei 3, kila mwaka Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza wamepewa mafunzo kuhusu sheria zinazosimamia taaluma yao.

Mafunzo hayo yametolewa leo na Mtandao wa mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria (TANLAP)  kwa kushirikiana na Chama cha wanasheria wanawake(TAWLA).

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa TANLAP, Christina Ruhinda, amesema  wameamua kutoa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari baada ya kufanya utafiti na kubaini  kwamba waandishi wengi wa habari wanakabiliwa na   changamoto ya uelewa wa sheria zinazosimamia tasnia ya habari.

Alisema waandishi wa habari ni msaada mkubwa kwenye jamii kwani huibu changamoto mbalimbali  hivyo wameona  kuna umuhimu wa kuwapa  mafunzo hayo yawasaidiea kutambua mipaka yao wanapotekeleza majukumu yao.

Naye Mwanasheria wa kujitegemea, ambaye pia alikuwa ni mwezeshaji katika mafunzo hayo, James Marenga aliwashauri waandishi wa habari kusoma sheria mbalimbali zinazohusiana na taaluma yao.

Alizitaja baadhi ya sheria zinazowahusu  ni pamoja  na sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016,  sheria ya haki ya kupata taarifa na sheria ya makosa ya mtandao za mwaka 2015 ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi huku wakijilinda.

“Epukeni kuingia kwenye mgogoro na sheria, sheria zipo na zinaishi tambueni kutokujua sheria hakukupi msamaha wa kutochukuliwa hatua za kisheria utakapotekeleza majukumu yako kinyume na sheria, ili kuepuka mgogoro huo ni wajihu wenu kuzisoma na kuzielewa sheria hizo,” alisema Marenga ambaye pia ni Mwandishi wa Habari Mwandamizi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC), Edwin Soko, aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuitumia vizuri elimu watakayoipata pia wawafikishie wenzao ambao hawajapata fursa ya kushiriki ili kwa pamoja waweze kufanya kazi katika mazingira Salama bila kuingia kwenye mgogoro na sheria.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Hellen Mtereko, alisema mafunzo hayo yamemsaidia kutambua tofauti kati ya uchochezi na kashfa hivyo uelewa huo utamsaidia kujiepusha kuandika habari za aina hiyo zitakazomuingiza kwenye mgogoro wa sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles