26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wenger ashitushwa na kiwango cha Rashford

Marcus RashfordMANCHESTER, ENGLAND

KOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, amedai kwamba ameshitushwa na uwezo wa nyota wa Manchester United, Marcus Rashford, aliouonesha juzi katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 18, juzi alionesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo huo dhidi ya Arsenal, ambapo alipachika mabao mawili ndani ya dakika tano katika kipindi cha kwanza kwenye ushindi wa mabao 3-2.

Kutokana na kiwango hicho, Wenger amedai kwamba hakutarajia kuona uwezo mkubwa ambao aliuonesha mchezaji huyo.

“Kwa upande wetu, tulishindwa kuwa na mipango mizuri ya kutafuta mabao kutokana na nafasi ambazo tulizipata, lakini katika mchezo huo nilikuja kushangazwa na uwezo wa nyota mpya wa Man United, Rashford.

“Nadhani haikuwa kwangu tu, ilikuwa kwa kila mmoja kushangazwa na uwezo wa mchezaji huyo ambaye alifanikiwa kufunga mabao mawili, alikuwa na akili ya kwenda na mchezo na kujua wapi sehemu sahihi ya kukaa.

“Ninaamini atakuja kuwa na uwezo wa hali ya juu endapo ataendelea na aina ya mchezo ambao anacheza na kama hatalewa sifa,” alisema Wenger.

Nyota huyo alianza kuonesha uwezo wake wa kupachika mabao katika mchezo wa Kombe la Europa dhidi ya Midtjylland, ambapo katika mchezo huo alifanikiwa kupachika mabao mawili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles