32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, February 2, 2023

Contact us: [email protected]

Klopp: Liverpool ilikosa bahati

jurgen-kloppLONDON, ENGLAND

BAADA ya Liverpool kupokea kichapo cha mabao 3-1 ya mikwaju ya penalti dhidi ya Manchester City, kocha wa klabu hiyo, Jurgen Klopp, amedai kwamba timu yake ilikosa bahati ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Katika mchezo huo wa Kombe la Capital One, dakika 90 zilimalizika huku timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, lakini Liverpool walikuja kutolewa katika matuta 3-1, na Klopp akidai kwamba walikosa bahati.

Mabao ya awali yaliwekwa wavuni na Philippe Coutinho kwa upande wa Liverpool, wakati Manchester City wakiwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mchezaji wake, Fernandinho.

“Nimeshangazwa na matokeo hayo, ninaamini tulikuwa na kila sababu ya kushinda fainali hiyo, ila tulikosa bahati japokuwa tulikuwa na nafasi nyingi za kupachika mabao.

“Nimejifunza mengi katika mchezo huo, ila kwa sasa ni kuangalia jinsi gani ambavyo tunaweza kusonga mbele katika michuano ya Ligi Kuu,” alisema Klopp.

Katika mchezo huo, mlinda mlango wa Man City, Willy Caballero, alionekana kuwa shujaa wa mchezo huo kwa kuokoa mikwaju mitatu ya penalti na kuifanya timu hiyo kutwaa ubingwa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles